Katika msimu uliopita ambao ndio huhesabiwa tuzo ya mwaka husika, Muleka alifunga jumla ya magoli 11 kwenye mashindano ya kimataifa, ambapo matatu yalikuwa kwenye timu ya taifa na mengine 8 yakiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe.
Tuzo hiyo ya mshambuliaji bora wa kimataifa hutolewa na International Federation of Football History and Statistics (IFFHS), ambapo kwa mwaka 2019 Ronaldo amechukua baada ya kufanikiwa kufunga magoli 14 akiwa na timu ya taifa ya Ureno na magoli 7 akiwa na Juventus kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji waliomfuatia Ronaldo ni Ali Mabkhout (United Arab Emirates), ambaye ana jumla ya magoli 19 kwenye michuano ya kimataifa pamoja na Harry Kane ambaye ana magoli 19 pia akifunga 12 na England na 7 akiwa na Tottenham kwenye ligi ya Mabingwa.
Ronaldo sasa ametwaa tuzo hiyo mara 5 ndani ya miaka 7 akianza mwaka 2013, 2014, 2016, 2017 na sasa 2019.
No comments:
Post a Comment