Uvumi unaoongezeka kuhusu mustakabali wa Paul Pogba baada ya ku
kosekana katika mazoezi ya kabla kuanza kwa msimu katika kambi ya Manchester United wiki hii.
Hii ni baada ya mchezaji huyo w akiungo cha kati wa Ufaransa kutumia ziara ya kibinfasi huko japan mwezi uliopita kueleza kwamba 'huenda sasa ni muda muafaka kutafuta changamoto mpya kwengineko'.
Lakini wakati wachezaji wenzake walifika kwa mazoezi hayo Jumatatu, Pogba hakufika na inaarifiwa ni kwa ruhusa ya meneja Ole Gunnar Solskjaer - baada ya kupewa muda wa mapumziko kufuatia miezi 16 ya pilka pilka.
Kauli kutoka United ni kwamba atakuwa kwenye ndege kuelekea Australia wakati kikosi cha kwanza kilipoelekea Perth Jumapili katika ziara ya kabla kuanza msimu.
Mustakabili wa Pogba umejadiliwa kwa miezi kadhaa - huku kukiwepo taarifa zilizosambaa kuhusu uhasama kati yake na aliyekuwa meneja wa United Jose Mourinho, huku mchezaji huyo akieleza mnamo Machi kwamba Real Madrid ni 'timu ambayo kila mchezaji angetamani kuichezea', licha ya kuongeza kwamba anafurahia kuwa Old Trafford.
Real na Juventus mara kwa mara zimehusishwa na Pogba, ambaye yuko kwenye mkataba na United hadi 2021. Kufikia sasa kumekuwa na ishara ndogo kutoka klabu zote hizo kwamba zitawasilisha pendekezo la kuishawishi United kumuuza kiungo huyo aliyeweka rekodi ya usajili wa thamani ya £ milioni 89.
Ratiba ya Pogba' tangu mwishoni mwa Mahi 2018 inaonyesha ni kwa namna gani ameruhusiwa mapumziko: aliichezea United mechi 10 za mwisho alafu akaichezea Ufaransa katika kiungo kikuu katika Kombe la dunia , na kufululiza moja kwa moja katika ligi kuu England.
Pamoja na Marcus Rashford na David de Gea, mchezaji huyo wa kiungo cha kati alicheza mechi 47 za klabu msimu uliopita na hakuna mchezaji wa United aliyemzidi.
Rashford na De Gea walipewa muda wa ziada wa kupumzika msimu huu wa joto na Pogba amekuwa na majukumu makubwa ya kimataifa katika msimu wa kuelekea 2019 kuliko wachezaji hao wawili akiichezea Ufaransa mechi tatu za dakika 90 kamili.
Kwa hivyo huku gumzo kuhusu mustakabali wa Pogba huko Man United ukiendelea angalau mpaka dirisha la uhamisho likifungwa England Agosti 8 - pengine angalau mpaka dirisha la uhamisho Italia likifungwa Agosti 23 au dirisha la uhamisho Uhispania Septemba 2 mtawalia, pengine kutokuwepo kwake katika mazoezi ssio sababu ya kuenea kwa uvumi huo.

No comments:
Post a Comment