Akizungumza baada ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Morogoro walioitaka Serikali kuweka bayana kama kupata vitambulisho vya taifa lazima ulipe hela, Naibu Waziri Masauni alisema vitambulisho hutolewa bure hakuna haja ya kulipa gharama yoyote huku akipiga marufuku wananchi kutozwa fedha nje ya ofisi za NIDA
“Kuanzia sasa kila Ofisi ya NIDA itakuwa na mawakili wa serikali wataohusika na kuandaa pamoja kuhakiki nyaraka mbalimbali za wananchi wanaokuja kwa ajili ya vitambulisho vya taifa” Masauni
“Ninatoa maelekezo kwa nchi nzima katika ofisi za NIDA kuwaondoa watu wanaowaandalia wananchi nyaraka hizo kwanza hatuwatambui kama ni maafisa sheria sahihi au la na wanaweza kuwathibitisha watu ambao sio raia wakapata vitambulisho kama raia” Masauni
No comments:
Post a Comment