Adbox

Thursday, January 2, 2020

Serikali yawagaia wakulima mbegu bora za zao la mchikichi

Wakulima wa michikichi mkoani kigoma wamefuraishwa na hatua  ya serikali kugawa bule mbegu za muda mfupi na zenye tija katika ukamuaji wa mafuta ya mawese ya zao la michikichi aina ya Tenela badala ya mbegu za zamani ambazo utumia zaidi ya miaka kumi mpaka kuanza uzalishaji.

Wakulima hao wamesema  mara baada ya taasisi ya utafiti wa kilimo nchini TARI kugawa zaidi ya mbegu 50,000 katika jeshi la Magereza Kwitanga kwa lengo la kutekeleza agizo la serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kuboresha uzalishaji wa zao la mchikichi ili kupunguza tatizo la kuagiza mafuta ya kula kutoka  nje ya nchi

Akikabidhi mbegu hizo kwa maafisa wa jeshi la magereza Kwitanga mkurugenzi mkuu wa TARI Dkr Geofrey Mkamilo amesema wameshaotesha mbegu za kisasa la zao la mchikichiki zaidi ya milioni 1.2 zenye uwezo wa kutoa mafuta kwa wingi na kuota kwa muda mfupi  ambazo zitagaiwa kwa wakulima na taasisi za serikali bule  na zimesaidia kuokoa zaidi ya bilioni 5.4 ambazo zingetumika kununua mbegu hizo.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa kilimo nchini TARI dkr Geofrey Mkamilo ambae ndio mratibu wa kuamasisha upandaji wa michikichi nchini amesema Tanzania inahitaji mafuta ya kula tani laki 570 huku yanayozalishwa nchini ni tani laki  205 na kusabaisha kutumia shilingi bilioni 443 kwaajili ya kuagiza tani  laki 365 ili kukidhi hali ya mafuta ya kula hapa nchini.

Ambapo uwoteshaji na Ugawaji wa miche  ya michikichi katika mkoa wa Kigoma kutokana na agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa unaendelea kwa kasi huku wanatarajia mpaka ifikapo June 2020 zaidi ya miche milioni 5 itakuwa imeoteshwa kwaajili ya kupewa wakulima.

No comments:

Post a Comment

Adbox