Adbox

Monday, December 30, 2019

Wanachama wa CHADEMA hawakutekwa walikamtwa na kuachiwa huru - Polisi Mwanza

Na James Timber-Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali zikidai kutekwa kwa wanachama wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Muliro Muliro amesema siku ya Desemba 29, Mwaka huu Majira ya 15:00 Mtaa wa Mahina Kata ya Mahina wilayani Nyamagana kulipatikana taarifa toka kwa raia wema kuwa kumeonekana watu wawili waliohisiwa kuwa siyo watu wema wakiwa karibu na Hoteli ya Paradise na kuingia nyumba jirani iliyokuwa karibu na hoteli hiyo.

Kamanda Muliro, amesema baada ya kupatikana taarifa hizo jeshi la polisi  lilifanya ufuatiliaji wa haraka na kufika eneo hilo na kuwakamata watu hao wawili, ambao katika mahojiano ya awali walikataa kutoa utambulisho wao kuwa wamefika maeneo hayo kufanya shughuli gani.

"Walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kati na kutoa ushirikiano kwa askari pia kutaja majina yao kuwa ni Abdukarimu Muro (31), mchaga Afisa Habari Katibu Mkuu CHADEMA Mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam na Said Haidani (30), Dereva wa Katibu Mkuu CHADEMA, Mkazi wa Mbezi Kimara Dar es Salaam wameambatana na Katibu Mkuu CHADEMA, Mh. John Mnyika na polisi waliwaachia baada ya kujiridhisha hawakuwa wahalifu waliachiwa huru," amesema ACP Muliro.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa onyo kwa kwa watu wasiokuwa na taarifa rasmi na wenye tabia za kuzusha mambo hasa ya watu wanapokamatwa wao husema kuwa wametekwa na hivyo kuzusha taharuki kwa jamii kwani matendo hayo ni makosa na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao watakapobainika.

No comments:

Post a Comment

Adbox