Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud wakati akifungua mkutano wa kutathimini mpango mkakati wa utekelezaji wa hifadhi ya Mtoto kwa kipindi Cha Miezi sita kupitia mradi wa UNICEF uliowashirikisha maafisa kutoka katika taasisi
mbalimbali za Mkoa.
Alisema umoja, ushirikiano na uadilifu wa taasisi hizo ndio njia pekee itakayowezesha kupiga hatua ya kupunguza na kuondoa vitendo hivyo kwani vinapelekea kuathiri mila, hulka na desturi za taifa.
Aliwataka watendaji hao kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake ili kuondosha malalamiko kwa wananchi.
Aidha alisema Serikali itachukua juhudi za kuzitafutilia kesi hizo na kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizobainika katika tathimini ya kikao hicho ambazo zinasababisha kukwamisha mwenendo mzima wa kesi za vitendo hivyo.
Hata hivyo aliwataka Wananchi kuacha kuvifumbia macho vitendo hivyo na badala yake waendelee kusimama imara katika kutoa ushahidi wa kesi hizo zinapofika Mahakamani ili kuisadia Mahakama Kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment