Tanzania imepiga bao kwenye maendeleo ya takwimu Afrika baada ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupongezwa kwa kuwa na takwimu bora na za kuaminika, Benki ya Dunia imebainisha hilo.
"Unapoangalia maendeleo ya takwimu barani Afrika, Tanzania imepiga hatua kubwa, tunapofuatilia uwezo wa takwimu duniani kote, NBS inafanya vizuri, kwa hiyo tunajivunia kufanya kani na ninyi (NBS), alisema Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Rob Swinkels wakati wa majadiliano ya Mpango wa Pili wa Taifa wa Takwimu.
Mchumi huyo Mwandamizi anayeshughulikia Umasikini na Mratibu wa Usawa kutoka benki hiyo, amepongeza Tanzania kwa kupiga hatua za kiuchumi zinazochagizwa na uwepo wa takwimu bora na za kuaminika zinazofanywa na NBS ambayo huwasaidia watunga sera kufanya maamuzi sahihi.
Alisema Tanzania ni moja ya nchi chache duniani ambazo zimepia hatua kwa ukuaji mzuri wa uchumi na ushujaa ulioshitua dunia na kwa hiyo Benki ya Dunia inajivunia kuwa na uhusiano mzuri na NBS.
Swinkels aliyeongoza ujumbe wa benki hiyo katika mkutano wa kuujengea uwezo Menejimenti ya NBS ulioanza Jumatatu wiki hii, alibainisha kuwa kuwa Tanzania inashika nafasi ya pili ikiifuatia Afrika Kusini kama nchi zilizo na takwimu bora katika Bara la Afrika. Aidha, Swinkels alitumia fursa hiyo kuelezea utayari wa Benki ya Dunia katika kuisaidia NBS katika kuandaa Mpango wa Taifa wa Takwimu (TSMP), hasa baada ya mpango wa kwanza kuwa na mafanikio makubwa.
Pia alibainisha kuwa Benki ya Dunia imeanzisha ushirikiano mpya na Jumuiya ya Afrika (AU) ili kusukuma mbele uwezo wa takwimu barani Afrika, kwa hivyo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazonufaika na ushirikiano huo.
Alisema Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Benki ya Dunia imetoa ruzuku ya dola za Marekani milioni 8.6 kwa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya takwimu na kuwa tayari imepitishwa na makubaliwa kwa ajili hiyo. Naye Mtakwimu Mkuu, Dk Albina Chuwa aliishukuru timu ya Benki ya Dunia kwa ushirika wenye manufaa katika kukamilisha uandaaji wa mpango huo.
Friday, November 1, 2019
Tanzania yang'ara Takwimu bora Afrika
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment