Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimewataka watumishi wa umma kuzitambua kanuni mpya zilizotolewa na mahakama za kuwatambua na kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalum pale wanapofika katika sekta zao.
Akizungumza katika semina iliyoandaliwa kwa mahakimu wa mahakama za mwanzo, wilaya, maofisa ustawi wa jamii na polisi wa dawati la jinsia kutoka Mkoa wa Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga, Ofisa Dawati la Makundi Maalum kutoka LHRC, Rose Nyatega amesema wamelazimika kutoa elimu kwa watumishi hao ili kuzitambua kanuni hizo.
Nyatega ambaye pia ni mwanasheria, alisema kanuni hizo zinaelekeza watu wenye mahitaji maalum wakiwamo albino, viziwi, watu wasioona, walemavu wa viungo, watoto na wajane wanapaswa kupewa kipaumbele na kuhudumiwa haraka pale wanapofika mahakamani, polisi na vituo vya maofisa ustawi wa jamii.
“Kwanza tunashukuru kutolewa kwa kanuni hizo za kutaka watu wenye mahitaji maalum kuhudumiwa haraka na kupewa kipaumbele, kama LHRC tunataka kuwapo na uwiano na kutokomeza ukatili wa jinsia, wanawake, watoto na hata wanaume wanafanyiwa ukatili lakini wanashindwa kudai haki zao hivyo lengo letu ni kuondoa dhana waliyojijengea ya kujinyanyapaa wenyewe.
“Tangu tuanze kutoa elimu kwa watumishi wa umma, tumebaini wapo baadhi yao hawajui kama kuna kanuni zimetolewa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ya kuhudumiwa haraka na kwa wakati, tatizo linguine tumebaini asilimia kubwa ya watu wenye mahitaji maalum nao wanajinyanyapaa wenyewe kwa kushindwa kudai haki zao ambapo wamejenga fikra potofu kwamba sheria zilizopo haziwahusu,”amesema Nyatega.
Ameongwza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia umeonekana kuwa mkubwa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa huku watoto na wanawake wakionekana kuathirika zaidi kuliko wanaume ingawa nao wananyanyaswa lakini wanaogopa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola na maamuzi wakihofia kuchekwa na jamii.
Friday, November 1, 2019
LHRC yawataka Watumishi wa umma kuwapa kipaumbele wenye mahitaji maalum
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment