Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi amewaasa Wanasheria wa Serikali katika Utumishi wa Umma kukubali mabadiliko, kubadilika na kujibadili vinginevyo jamii itawabadili.
Ameyasema hayo jijini Dodoma, wakati akihitimisha kikao kazi cha siku mbili baina yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya huduma za kisheria kutoka Wizara, Mashirika, Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Taasisi mbalimbali za serikali.
“Tumekutana hapa kwa siku mbili, tumejadiliana mafanikio na changamoto zinazotukabili katika taaluma yetu, tumebadilishana mawazo ili sote tuwe na picha ya pamoja, niwashukuru kwa michango yenu, mawazo yenu na na mapendekezo yenu sura moja na lengo letu ni moja tu tunajenga nyumba moja ambayo ni serikali ambayo mwisho wa siku tuijengee nchi yetu na watu wake na hii nchi inamatarajio yake, inamatumaini yake na sisi ni sehemu ya mchakatao huo”.
"Lakini niseme kwa namna moja au nyingine picha ya wanasheria katika jamii siyo nzuri sana, tunaweza kuwazungumzia mawakili wa kujitegemea lakini pia wanasheria wa serikali wamo
katika mkumbo huo," amesema Mwanasheria Mkuu.
Na kwa sababu hiyo akawataka wanasheria hao wa Serikali kwamba wanalazimika kubadilika tusipobadilika tutabadirishwa na jamii, tutabadilishwa na mazingira na hii ni kwa wanasheria wote hata mawakili wa kujitegemea “Profesa Kilangi akabainisha kwa kusema mtu wa mtaani anaangalia namna gani haki inatendeka, namna gani mambo yanayomgusa katika maisha yake yanathaminiwa na kutekelezwa kwa misingi ya haki, haangalii mbwembwe zako au lugha unayoongea hayo hayamhusu anataka haki itendeke kwa hiyo kubadirika ni lazima, kujibadilisha ni wajibu na lakini ili ufanye mabadiriko yatakayokuacha salama lazima ujitengenezee utaratibu unataka ubadirike vipi na kwa namnma gani na ndiyo sababu ya kukutana hapa kwa siku mbili”.
Amewaeleza Wanasheria hao katika utumishi wa umma kwamba serikali na nchi kwa ujumla imo katika mabadiliko makubwa. “Na sisi ni sehemu ya mchakato huo wa kuijenga nchi na hasa kushughulikia matatizo ya watu katika eneo hili la sheria”.
Akizungumzia zaidi kuhusu mabadiriko, Profesa kilangi amesema, mabadiliko huambatana na wasiwasi na taharuki na kwamba hata miongoni mwa wanasheria hao wa serikali wapo wenye wasiwasi lakini akawahakikishia kwamba mabadiriko hayo hayalengi katika kumkomoa mtu bali ni katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yao na kuwajengea mazingira bora zaidi kama Wanasheria wa Serikali.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Bw. Eustard Ngatale amemshukurua Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuandaa kikao kazi hicho na kuomba Miongozo mbalimbali iliyowasilishwa kwao ikamilike haraka ili waweze kuitumia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Rasimu ya Miongozo iliyowasilishwa kwa Wanasheria hao ni Muongozo wa kutunga sheria ndogo;Muongozo ya upekuzi wa Mikataba mbalimbali;Muongozo wa majadiliano ya Mikataba yote. Muongozo wa usimamizi wa utekelezaji wa Mikataba na Muongozo wa utoaji wa ushauri wa kisheria.
Vile vile katika kikao kazi hiki wanasheria wa Serikali walisitizwa kuhakikisha kwamba hukumu zinazotolewa na mahakama baada ya kesi kumalizika zinatekelezwa ili kuepuka matatizo yanayotokana na kutotekelezwa kwa hukumu hizo.
Friday, November 1, 2019
Mwanasheria Mkuu wa Serikali awataka wanasheria kukubali mabadiliko
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment