Adbox

Monday, July 22, 2019

Tetesi za Soka leo 22/07/2019



Real MadridHaki miliki ya pichamapigo.com

Klabu ya ligi ya Uchina Beijing Guoan wamepania kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale. Klabu hiyo, ina mpango wa kumfanya winga huyo mwenye miaka 30 kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uchina. (telegraph)
Manchester United, ambao awali walikuwa wakimnyemelea Bale wamejitoa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo. (Manchester Evening News).
Man United hatimaye imekubali masharti ya kumsajili beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atawasili katika uwanja wa Old Trafford kwa dau la £80m . (Bleacher Report)
  • Pacquiao ashinda ubingwa wa dunia akiwa na umri wa miaka 40


  • Tetesi za soka Ulaya Jumapili 21.07.2017
  • Droo ya kombe la mataifa ya Afrika 2021 yakamilika
  • Harry MaguireHaki miliki ya pichamapigo.com

    Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Kolscielny amekubali kujiunga na klabu ya Rennes. (RMC Sport).
    Arsenal inatarajiwa kuishinda Tottenham katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos. Mchezaji huyo wa Uhispania atajiunga kwa mkopo.(Mirror)
    Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza James Milner ,33, amesema hajui hatma yake katika klabu hiyo licha ya kwamba anataka kusalia. (Liverpool Echo)


    James MilnerHaki miliki ya pichamapigo.com

    Bayern Munich wanapigiwa upatu kumsaini winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha ,26, baada ya kushindwa kumsaini Leroy Sane na Gareth Bale. (90min)
    Ombi la Crystal Palace la £20m kumsaini beki wa Uingereza Reece James limekataliwa na Chelsea. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alihudumu msimu uliopita akiichezea Wigan.(Star)
    Arsenal, Chelsea, Manchester United na West Ham wote wana hamu ya kumsajili mchezaji wa Dynamo Kiev na Ukraine Mykola Shaparenko. (Caught Offside)


    Wilfried Zaha

    Real Madrid wamekataa ofa sita za kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, ambaye anahusishwa na uhamsho wa kuelekea Liverpool. (Cadena SAR)

    No comments:

    Post a Comment

    Adbox