Waziri mkuu wa Uingereza ataongoza kikao cha kamati ya dharura siku ya Jumatatu baada ya meli ya mafuta iliokua ikipeperusha bendera ya Uingereza kukamatwa na Iran katika Ghuba.
Theresa May anatarajiwa kupokea taarifa kutoka kwa mawaziri na maafisa na kuzungumzia umuhimu wa kuzipatia usalama wa kutosha meli katika eneo hilo.
Hatua hiyo inajiri kufuatia ripoti kwamba mawaziri wanapanga kupiga tanji mali ya Iran.
- Majibizano kati ya majeshi ya Iran na yale ya Uingereza yafichuliwa
- Uvamizi wa al-shabab: Wakaazi wawaokoa wenzao
- Tazama Video ya majibizano kati ya majeshi ya Iran na yale ya Uingereza
Waziri wa maswala ya kigeni Jeremy Hunt anatarajiwa kuwajuza wabunge baadaye kuhusu hatua ambazo seriikali ya taifa hilo itachukua.
Siku ya Jumapili , afisi ya wizara ya maswala ya kigeni ilithibitisha kwamba bwana Hunt alizungumza na wenzake wa Ujerumani na Ufaransa ambao wote wameshutumu vitendo vya Iran.
Bwana Hunt aliwashukuru mawaziri wa maswala ya kigeni Jean Yve Le Drian na waziri wa kigeni nchini Ujerumani Heiko Maas kwa kuunga mkono Uingereza.
Mawaziri wote walikubaliana kwamba kuna umuhimu wa kuimarishwa kwa usalama katika eneo hilo ili meli kuweza kupita katika mkondo wa bahari wa Hormuz kwa usalama huku ikizuia hatari yoyote ya mgogoro kutibuka katika eneo hilo.
Mawaziri wamekana madai kwamba serikali imepuuza hali inayoendelea katika eneo la Ghuba kutokana na siasa za nyumbani.
Chansela Phillip Hammond amesisitiza kuwa serikali imekuwa ikifanya mazungumzo na Marekani pamoja na washirika wake wa Ulaya ili kujibu vitendo vya Iran katika kipindi cha miezi kadhaa.
Na waziri wa ulinzi Tobias Ellwood alisema kuwa Uingereza ilikuwa na meli ambazo zimekuwa zikipitia mkondo huo kila siku na kwamba ni vigumu kuzisindikiza meli zote.
Alipendekeza kwamba fedha zaidi zinafaa kuwekezwa katika jeshi la wanamaji wa Uingereza ili kuliwezesha kushiriki vyema katika ulingo wa kimataifa.
Je wanasiasa wa Uingereza wanasema nini?
Akizungumza katika kipindi cha BBC , bwana Hammond alisema kwamba Uingereza itatumia kila njia ya kidiplomasia ili kutatua mzozo huo.
Alisema kwamba vikwazo , ikiwemo vile vya kifedha dhidi ya Iran tayari vimewekwa na haijajulikani ni nini zaidi kinachohitajika kufanywa.
Lakini bwana Dancun Smith aliambia BBC kulikuwa na maswali ambayo yalihitaji kuulizwa kuhusu vitendo vya seriikali ya Uingereza.
Alisema kwamba kuzuiliwa kwa meli ya mafuta ya Iran wiki mbili zilizopita kulifaa kuwa onyo kwamba meli za Uingereza zinazopitia Ghuba zilihitaji kupatiwa usalama.
Nini kilichotokea?
Stena Impero ilikamatwa na wanajeshi wa Iran al maarufu Iranian Revolutionary Guard siku ya Ijumaa katika eneo muhimu la maji katika Ghuba.
Meli hiyo ya mafuta ilizingirwa na meli nne na helikopta kabla ya kuelekezwa katika eneo la maji la Iran, amesema Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt.
Amesema kuwa "kuhusu kusafiri majini lazima uimarishwe" na akaonya kuwa itakuwa na " athari mbaya " kama hali haitatatuliwa haraka..
" Hatuangalii hatua za kijeshi ," na kuongeza kuwa: "Tunatafuta njia za kidiplomasia za kutatua hali hii."
Meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose iliarifiwa lakini ilikuwa mbali sana kuweza kuzuia utekaji huo.
Majibizano kati ya wanajeshi wa Uingereza na wanajeshi wa Iran yaliofanyika kabla ya meli hiyo kukamatwa yalifichuliwa.
Katika sauti zilizorekodiwa meli ya Iran ilisikika ikiiambia meli ya MHS Montrose kwamba inataka kuipekua meli ya Stena Impero kwa maswala ya kiusalama.
Kitengo cha habari cha Iran IRNA kilisema kuwa meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya kugongana na boti ya uvuvi na kukataa kuitikia mwito wa meli hiyo ya wavuvi.
Lakini bwana Hunt alisema kuwa meli hiyo ilikamatwa katika maji ya Oman katika ukiukaji wa sheriza za kimataifa na kulazimishwa kuelekea katika bandari ya Bandar Abbas nchini Iran.
Mmmiliki wa meli hiyo Stena Bulk anasema kwamba amewasilisha ombi rasmi la kuwatembelea wafanyakazi wa meli hiyo.
Je Iran imesema nini?
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif alituma ujumbe katika mtandao wake wa twitter akisema kwamba Uingereza inafaa kukoma kuwa gaidi wa kiuchumi wa Marekani.
Alisema kwamba Iran inawahakikishia usalama wote katika mkondo wa Hormuz na kusisitiza kuwa vitendo vyake ikisema inafuata sheria za majini.
Balozi wa Iran nchini Uingereza ameionya Uingereza dhidi ya kusababisha mgogoro na wasiwasi katika eneo hilo. Hamid Baeidinejad alisema katika Twitter:
Ni kitendo cha hatari kisicho na busara wakati huu. Iran hatahivyo iko imara na tayari kwa hatua yoyote.
Nini chanzo cha yote haya?
Tukio hili limefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Uingereza, Marekani na Iran.
Jeshi limesema meli hiyo imekamatwa kwa kuvunjwa kwa sheria tatu: kuzima GPS; kuingia kwenye mpaka kupitia njia ya kutokea badala ya kuingilia; na kupuuzia maonyo.
Taarifa zinasema hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi na usalama wa wafanyakazi ni jambo la kwanza kwa wamiliki na mameneja.
Tarehe 9 mwezi Julai, Uingereza ilieleza tishio la usalama katika maji ya Iran kwenye Ghuba ni ''kubwa''.
'Marekani haiwezi kuizuia Iran kuuza mafuta'
Wakati huohuo, Marekani imedai kuwa imedungua ndege isiyo na rubani kwenye Ghuba, baada ya Iran kushambulia ndege isiyo na rubani katika eneo hilo mwezi Juni.
Raisi wa Marekani Donald Trump amesema atazungumza na Uingereza kufuatia madai kuwa Iran imeikamata meli iliyosajiliwa nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment