Sauti zilizorekodiwa zimebaini majibizano makali kati ya wanamaji wa Uingereza na wanajeshi wa Iran waliokua ndani ya meli ya kijeshi, muda mfupi kabla ya meli ya mafuta iliokuwa na bendera ya Uingereza kukakamtwa katika Ghuba.
Katika sauti hizo , meli ya Iran iliambia meli hiyo ya majeshi ya Uingereza kwa jina MHS Montrose kwamba inataka kuipekua meli hiyo kwa maswala ya kiusalama.
Chansela Phillipa Hammond alisema kuwa serikali itatumia njia zote za kidiplomasia kutafuta suluhu.
- Iran imesema video yao inaonyesha 'ndege haikudunguliwa'
- Vita kati ya Iran na Marekani 'haitatokea'
- Iran: Marekani inatusingizia
Lakini balozi wa Iran mjini London aliionya Uingereza dhidi ya kusababisha mgogoro.
Hamid Baeidinejad alisema katika twitter yake kwamba: Hii ni hatari sana na sio busara wakati kama huu katika eneo hilo.
Iran hata hivyo ni imara na iko tayari kwa matukio yoyote.
waziri huyo wa maswala ya kigeni ameitaka Iran kuiwachilia meli hiyo. Anayodai ilikamatwa kwa njia ya haramu.
Jeremy Hunt amesema kuwa wabunge wataarifiwa siku ya Jumatatu kuhusu hatua zitakazochukuliwa na serikali.
Nini kilichotokea
Stena Impero ilikamatwa na wanajeshi wa Iran al maarufu Iranian Revolutionary Guard siku ya Ijumaa katika eneo muhimu la maji katika Ghuba.
Meli hiyo ya mafuta ilizingirwa na meli nne na helikopta kabla ya kuelekezwa katika eneo la maji la Iran, amesema Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt.
Amesema kuwa "uhusu wa kusafiri majina lazima uimarishwe" na akaonya kuwa itakuwa na " athari mbaya " kama hali haitatatuliwa haraka..
" Hatuangalii hatua za kijeshi ," na kuongeza kuwa: "Tunatafuta njia za kidiplomasia za kutatua hali hii."
- Trump asitisha mashambulizi dhidi ya Iran 'dakika za mwisho'
- Marekani yakiri ndege yake kutunguliwa na Iran
Jumamosi Bwana Hunt alituma ujume wa twitter uliosema: " hatua ya jana katika eneo la Ghuba inaonyesha ishara za wasi wasi , Iran inaweza kuwa inmechukua mkondo hatari wa kuyumbisha hali kinyume cha sheria baada ya kumamatwa kwa meli ya mafuta katika eneo la Gibraltar kuelekea Syria."
Shirika la habari linalomilikiwa na taifa la Iran IRNA limesema kuwa meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya kugongana na boti la uvuvi na kushindwa kujibu mawasiliano ya meli nyingine ndogo.
Mmiliki wa meli hiyo alisema kuwa ilikuwa inatekeleza kikamilifu masharti na sheria na ilikuwa katika eneo la maji la kimataifa ilipovamiwa na kutekwa.
Imesema kuwa hakuna taarifa za majeruhi miongoni mwa wahudumu wa meli hiyo 23, ambao walikuwa uraia wa mataifa ya India, Urusi, Latvian na Ufilipino.
Msemaji wa serikali ya Uingereza ameiambia BBC kuwa : "tumeshauri meli za mizigo za Uingereza kuwa mbali na eneo la Ghuba kwa muda ."Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London.
''Balozi wetu mjini Tehran anfanya mawasiliano na wizara ya mambo ya kigeni wa Iran kutatua hali hii na tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kimataifa,'' alisema.
Ni nini kilichorekodiwa?
Katika sauti zilizorekodiwa , meli ya Iran ilisikika ikiambia meli moja iliodaiwa kuwa Stena Impero -kubadilisha mkondo wake , ikisema kuwa iwapo utaheshimu utakuwa salama.
HMS Montrose inajitambulisha katika sauti hiyo iliopatikana na kampuni ya Uingereza kuhusu usalama wa majini Dryad Global.
Inaambia meli ya Stena Impero: wakati unaposafirisha mizigo katika mkondo wa bahari wa kimataifa na chini ya sheria za safari yako haifai kukatizwa ama kuzuiwa.
Baadaye meli hiyo inakiuliza chombo hicho cha Iran kuthibitisha hakina lengo la kukiuka sheria za kimataifa kwa kujaribu kupanda ndani ya meli hiyo.
Nini chanzo cha yote haya?
Tukio hili limefanyika wakati kukiwa na mvutano kati ya Uingereza, Marekani na Iran.
Jeshi limesema meli hiyo imekamatwa kwa kuvunjwa kwa sheria tatu: kuzima GPS; kuingia kwenye mpaka kupitia njia ya kutokea badala ya kuingilia; na kupuuzia maonyo.
Taarifa zinasema hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi na usalama wa wafanyakazi ni jambo la kwanza kwa wamiliki na mameneja.
Tarehe 9 mwezi Julai, Uingereza ilieleza tishio la usalama katika maji ya Iran kwenye Ghuba ni ''kubwa''.
Wakati huohuo, Marekani imedai kuwa imedungua ndege isiyo na rubani kwenye Ghuba, baada ya Iran kushambulia ndege isiyo na rubani katika eneo hilo mwezi Juni.
Raisi wa Marekani Donald Trump amesema atazungumza na Uingereza kufuatia madai kuwa Iran imeikamata meli iliyosajiliwa nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment