Timu mbili za Afrika magharibi zinashuka dimbani leo katika uwanja wa Alexandria Misri zote zikiwania nafasi katika robo fainali.
Super Eagles ya Nigeria na Indomitable Lions ya Cameroon zinapambana kuitafuta nafasi hiyo ya robo fainali katika mashindano yanayoendelea ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon
SuperEagles imeshinda mechi 6 kati ya 7 zilizopita katika mashindano ya AFCON na Indomitable Lions nayo ikiwa haijawahi kushindwa katika mechi 9 zilizopita za AFCON kwa mujibu wa shirikisho la soka barani Afrika Caf
- Senegal na Benin zatinga robo fainali Afcon
- Cheza: Nani mshindi AFCON kwa mambo mengine kando na soka?
- Kutolewa mapema Afcon ni somo kwa Tanzania - Amunike
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Nigeria, Wilfred Ndidi anadhani kwamba huenda Cameroon akawa mpinzani mwepesi kuliko Madagascar, iliyowashinda katika mechi ya mwisho katika makundi.
Cameroon inakabiliwa na kibarua kigumu leo kutokana na kwamba imeshindwa kujipatia magoli yanayohitajika, na pia ari kubwa iliopo kwa upande wa Nigeria katika kutaka kuacha ujumbe mzito baada ya kipigo cha Madagascar.
No comments:
Post a Comment