Jumuiya kujihami ya NATO inasema hakuna dalili ya Urusi kusalimu amri katika mgogoro wa makombora. Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameonya kwamba nafasi ya kuukoa mkataba kuhusu silahauliofikiwa wakati wa vita baridi inapungua kila siku.
Kauli ya Stoltenberg imekuja baada ya kufanyika mazungumzo na maafisa wa Urusi ambayo yameshindwa kufikia mwafaka wa aina yoyote. Urusi na Marekani zote zilisitisha hatua ya kushiriki kwenye mkataba wa kuondowa makombora ya Nyuklia ya masafa ya kati kila mmoja akimtuhumu mwenzie kwamba amekiuka mkataba huo ambao kimsingi ulipiga marufuku matumizi ya makombora yote ya Nuklia ya uwezo wa kati.
Marekani hakuna shaka kwamba itajiondowa kwenye mkataba huo mwezi Agosti ikiwa Urusi haitoharibu mfumo wake tata wa makombora ambao Marekani na jumuiya ya NATO zinasema unakiuka makubnaliano yaliyosainiwa mwaka 1987 kati ya rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa Soviet Mikhail Gorbachev.
No comments:
Post a Comment