Kamanda cha kikosi cha usalama barabarani nchini ACP Fortunatus Muslim amekutana na chama cha wakala wa utalii Tanzania (TATO) pamoja waongoza watalii kujadili changamoto na kero mbalimbali wanazokutana nayo katika sekta hiyo
Kikao hicho ni muendelezo wa vikao vya kukutana na wadau wa usafirishaji kufuatilia changamoto katika sekta ya usafirishaji wa abiria na upande wa Utalii.
Aidha ziara hiyo ya kamanda ni kutokana na maelekezo ya waziri mkuu Kasim Majaliwa aliyoyatoa katika kikao alichokutana na wafanyabiashara wa mabasi ambapo waliwasilisa changamoto ambazo Kamanda Muslim alitakiwa azifanyie kazi kwa kutembelea katika mikoa ya Manyara na Arusha ili kuyafanyia ufumbuzi
Changamoto hizo zilizojitokeza mkoani Manyara ni suala la usajili wa magari ya Noah na aina ya haice na uhamishwaji wa stand ya zamani kwenda stand mpya na kuwepo kwa askari wachache wasio na madili ambao wamekuwa ni kero wafanyabiashara.
Katika mkoa wa Arusha Changamoto iliyojitokeza ni kusimamishwa mara kwa mara kwa magari ya utalii na Kamanda Muslim amesema kupitia vituo hivyo sasa njia mbadala imepatikana
Akiwa na wadau hao amesema changamoto zilizojitokeza zimefanyiwa kazi na tayari katika mkoa huo kuna maeneo manne yametengwa kwa ajili ya ukaguzi ambayo yatatumika kwa ajili ya ukaguzi wa magai ya utalii ambayo yataonekana yana matatizo na yale ambayo hayana matatizo yataendelea na safari na vituo vitatumika kutolea taarifa ambazo zitafanyiwa kazi na polisi.
Aidha ameelekeza magari ya watalii yakaguliwe katika maeneo rasmi yatakayotengwa na magari hayo yaorodhereshwe ili wakaguzi waende kuyakagua ili kubandika stika ya usalama ili kuondoa usumbufu wa kusimama barabarani kwa ajili ya ukaguzi.
Pia ameelekeza kwamba kuwa magari ya utalii yanayodaiwa faini wawasiliane na kampuni kampuni husika badala ya kusubiri magari ya utalii kusimamishwa barabarani kwa kuwa watalii hawafahamu matatizo yaliopo.
Kwa pamoja wamekubaliana kuwa vituo vitumike na tayari makontena yameshatengenezwa kwa ajili ya kuwekwa katika vituo ambapo vitatumika kama ofisi ambapo kamanda aliviona na Tato wamenunua gari jipya ambalo litatumika katika uangalizi wa usalama wa wawatalii na tayari mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro ameshalipa kodi ya gari hilo
Aidha wamekubaliana Tato itaanda mafunzo kwa ajili ya askari wa usalama barabarabani ili kuwajengea uelewa wa masuala ya usalama barabarani.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa TATO Mhe. Sirili Akko amesema kuwa changamoto katika sekta ya utalii ni kubwa hasa upande wa usalama barabarani ambapo wakaona ni vema kuweka utaratibu kwa kushirikiana na serikali ili kuweka vituo hivyo vya Ukaguzi.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Usalama barabarani Tanzani amesema kuwa wao kama Wadau wa utalii wamefanya utafiti mtalii anapoanza safari kutoka uwanja wa KIA mpaka geti la kuingia Ngorongoro gari la watalii linaweza kusimamishwa na askari zaidi ya mara 20 jambo ambalo kwasasa limeshughulikiwa tofauti na ilivyokuwa.
Aidha Muslimu amesema atahakikisha anashirikiana na wadau hao kutatua changamoto zote za watalii ili wageni wanapokuja nchini waone ni mahali salama na ambapo hawatapata bughudha kutokana na Askari huku akiwasihi wamiliki wamakampuni wa kitalii kuajiri madreva wenye vigezo vya kuendesha watalii

No comments:
Post a Comment