Bill Gates ni bilionea wa pili duniani kulingana na jarida la Forbes akiwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 103. Alianzisha kampuni ya Microsoft mnamo mwaka 1975 na rafiki yake wa utotoni Paul Allen.
Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, ametangaza kujiuzulu kutoka kwenye bodi ya kampuni hiyo na kujielekeza zaidi katika shughuli zake za uhisani.
Kwenye taarifa yake, bilionea huyo amesema anataka kuwekeza muda zaidi katika masuala ya afya ulimwenguni, elimu na mabadiliko ya tabia nchi. Gates, ambaye aliifanya Microsoft kuwa mojawapo ya kampuni ya teknolojia yenye thamani kubwa duniani, alijiondoa katika majukumu ya utendaji mwaka 2008, ili kutumia muda zaidi katika taasisi yake ya kutoa misaada ya Bill na Melinda, ambayo anaiendesha pamoja na mke wake.
Bill Gates ni bilionea wa pili duniani kulingana na jarida la Forbes akiwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 103. Alianzisha kampuni ya Microsoft mnamo mwaka 1975 na rafiki yake wa utotoni Paul Allen.
Bill Gates ni bilionea wa pili duniani kulingana na jarida la Forbes akiwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 103. Alianzisha kampuni ya Microsoft mnamo mwaka 1975 na rafiki yake wa utotoni Paul Allen.

No comments:
Post a Comment