Bora, Kapteni Mstaafu, George Huruma Mkuchika amezielekeza
Halmashauri za Wilaya zote nchini kwa kushirikiana na Mpango wa
kuanzisha Vituo vya Urasimishaji na Uendelezaji Biashara (One Stop
Business Formalization and Development Centers) katika maeneo yao kwa
nia ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara ili biashara zao ziwe rasmi na
kuendesha kwenye mfumo unaotambulika kisheria.
Mkuchika
ameyasema hayo akiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Selikari za Mitaa wakati wakikagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na
kamati hiyo kwenye ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Singida, kwenye
kituo cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kilichoanzishwa na
Manispaa ya Singida kwa kushirikiana na MKURABITA wakati alipokuwa
akiongea na wafanyabiashara na vikundi vya wajasiliamali mbalimbali wa
Singida.
Amesema amefurahishwa na ubunifu uliofanywa na
Manispaa ya Singida kwa kuanzisha kituo hicho ambacho ni msaada mkubwa
kwa ajili ya kuwakwamua wafanyabiashara na kuzitaka Halmashauri nyingine
kuja kujifunza namna ya kuanzisha vituo hivyo kutoka Manispaa ya
Singida kwa kuwa kimekuwa kikifanya kazi zake vizuri.
“Niseme
wazi tumefurahishwa sana na ubunifu mlioufanya kwa kuanzisha kituo
hiki kwa kuwa ni jambo muhimu sana linalotakiwa kwa wakati wa sasa
kwa maendeleo ya taifa letu”alisisitiza Mkuchika
Akitoa taarifa
ya kituo hicho mbele ya Kamati, Afisa Biashara wa Manispaa ya
Singida, Erick Sinkwembe amesema katika mwaka 2018/2019 Manispaa ya
Singida kwa kushirikiana na MKURABITA wamefanya urasimishaji biashara
kwa njia ya kujenga uwezo kwa wafanyabiashara 777.
Amesema
lengo kuu la kuanzisha kituo hicho ni kufanya mchakato mzima wa
urasimishaji wa biashara kuwa wa haraka ,rahisi na wa gharama nafuu kwa
mfanyabiashara ambapo aliongeza kwamba shughuli za urasimishaji
biashara kwenye Manispaa ya Singida zimefanywa kwa kushirikiana na
wadau kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
Amezitaja
taasisi hizo kuwa ni Benki ya NBC,CRDB na NMB,BRELA,NSSF,SIDO,TCCIA,NIC,
TRA pamoja na NHIF na kwamba shughuli za Kituo hicho zilianza rasmi
tarehe 10/12/2019 ambapo Ofisi ya Biashara ya Manispaa pia
ilihamishiwa hapo ili kurahisisha utendaji kazi
Amesema awali
jengo hilo ambalo linatumika kama kituo lilikuwa ukumbi wa Manispaa
na baada ya kukarabatiwa na Manispaa kwa jumla ya shilingi
17,349,960/= na MKURABITA kuwezesha vitendea kazi (Komputa, UPS,Scanner
na Printa) vyenye jumla ya gharama ya shilingi 4,071,000/= limeweza
kufanya kazi ambapo amesema kilichobaki ni kuunganisha mfumo wa TEHEMA
utakaogharimu jumla ya shilingi 3,995,000/=, kazi ambayo amesema
itakamilika katika siku chache zijazo.
Mratibu wa Programu ya
MKURABITA nchini, Dkt. Seraphia Mgembe ameitaka Ofisi ya Biashara ya
Manispaa ya Singida kuwa kiungo kikuu baina ya wadau katika mnyororo
mzima wa urasimishaji na uendelezaji wa biashara kwenye Manispaa hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Dkt. Jasson Rweikiza amesema Kamati yake imeridhishwa
na kazi inayofanywa na Kituo hicho na kuwataka wafanya biashara
kutumia fursa hiyo vizuri kupata mikopo katika Taasisi za kifedha ili
kuziendeleza biashara zao.
Kwa nyakati tofauti wajasiliamali na
wafanyabishara wameomba kamati kuangalia namna ambavyo Serikali
itakavyowapunguzia kodi ambapo pia waliomba watumishi wa taasisi zote
kuwepo katika kituo hicho ili kuwarahisishia kupata huduma zote kwa
wakati mmoja na kwa haraka.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.
Rehema Nchimbi ameishukuru Kamati kwa michango yao waliyotoa ili
kuboresha kituo na miradi yote waliyoikagua katika ziara yao ya siku
mbili ambapo amesema Mkoa umepokea na utafanyia kazi kikamilifu
maelekezo yote yaliyotolewa ili kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi
wa mkoa wa Singida kama kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu!
Katibu
Tawala Mkoa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi amesema katika ziara hiyo
kamati imeweza kukagua miradi mbalimbali ambayo ni Ukarabati wa Shule
ya Sekondari Mwenge kupitia mpango wa ukarabati wa shule kongwe za
Serikali (89),Mradi wa Timiza Malengo unaosimimamiwa na kufadhiliwa na
TASAF, Kituo cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara, Eneo la ujenzi
wa Chuo Cha Utumishi wa Umma (Mungumaji) Kampasi ya Singida na Ujenzi
wa barabara kiwango cha lami unaofanywa na Wakala wa Barabara Mjini na
Vijijini (TARURA).

No comments:
Post a Comment