Meli ya mafuta iliokamatwa na Iran: Waziri Jeremy Hunt aomba usaidizi kutoka nchi za Ulaya
Wizara ya maswala ya kigeni imesisitiza wito wake wa kuitaka Iran kuiwachilia meli iliokuwa ikipeperusha bendera yake inayozuiwa na jeshi la Iran pamoja na wafanyikazi wake.
Jeshi ya Revoliutionary Guard liliikamata meli hiyo ya Stena Impero na wafanayakazi wake 23 katika eneo la Ghuba siku ya Ijumaa.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingreza aliliambia bunge kwamba kilikuwa kitendo cha uharamia. Bwana Hunt alisema kwamba Uingereza itabuni ujumbe wa usalama wa majini na mataifa mengine ya Ulaya ili kuwezesha meli kupita katika eneo hilo zikiwa salama.
- Majasusi wa 'Marekani kunyongwa' Iran
- Mzee Mwinyi akerwa na January Makamba
- Mtembo: Mti wa usuluhisho huko Mwika Tanzania
Waziri huyo alipata uungwaji mkono kuhusu mpango huo kutoka kwa Ufaransa na Ujerumani siku ya Jumapili, BBC imeambiwa.
Akiwahtubia wabunge hao baada ya mkutano na kamati ya kushughulikia maswala ya dharura kwa jina Cobra, bwana Hunt alisema kwamba alizungumza akiwa na moyo mzito , lakini akaonya kwamba iwapo Iran itaendelea kufanya vitendo inavyofanya italazimika kukubali idadi kubwa ya majeshi ya Ulaya katika pwani yake.
Kukamatwa kwa Stena Impero katika mkondo muhimu wa uchukuzi wa meli wa Hormuz unajiri baada ya Tehran kusema kwamba meli hiyo ilikiuka sheria za majini.
Chombo cha habari nchini Iran kimesema kwamba meli hiyo ya mafuta ilikamatwa baada ya kugongana na boti ya wavuvi na kukataa kujibu wito wa boti hiyo.
Bwana Hunt anasema kuwa meli hiyo ilikamatwa kwa njia isiofaa katika maji ya Omani na kulazimishwa kuelekea katika bandari ya Abbas nchini Iran, ambapo ipo hadi kufikia sasa.
- Majibizano kati ya majeshi ya Iran na yale ya Uingereza yafichuliwa
- Tazama Jinsi majeshi ya Iran yalivyoikamata meli ya Uingereza
Ijapokuwa wamiliki na wafanyakazi wa meli hiyo sio Waingereza , Stena Impero inabeba bendera ya Uingereza hivyobasi Uingereza inafaa kuipatia ulinzi, kulingana na wachanganuzi wa wa maswala ya majini.
Kukamatwa kwa meli hiyo ndio kisa cha hivi karibuni kilichosababisha hali ya wasiwasi kati ya Iran, Uingereza na Marekani.
Mapema mwezi huu wanamamaji wa Uingereza waliisaidia kukamatwa kwa meli ya mafuta ya Grace 1 ya Gibraltar kwa kuwa kulikuwa na ushahidi kwamba ilikuwa ikibeba mafuta ya Iran kulekea Syria hatua inayokiuka vikwazo vya EU.
Bwana Hunt alisema kwamba meli hiyo ilikamatwa kwa njia halali, lakini Iran ikasema kwamba ni uharamia na kutishia kuikamata meli ya Uingereza ili kulipiza kisasi.
Katika taarifa kwa wabunge , bwana hunt alisema kwamba Uingereza itaunda ujumbe wa majeshi ya Ulaya ili kuhakiukisha kuwa eneo hilo ni salama kwa uchukuzi wa meli za kimataifa.
''Uhuru wa uchukuzi wa majini ni muhimu kwa kila taifa'', alisema. Idara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa itabuni jeshi la kimataifa la majini ili kutoa utatuzi wa hali hiyo.
Lakini ujumbe huo wa Uingereza umesema kuwa hautaishirikisha Marekani kwa sababu bwana Hunt anasisitiza Uingereza haiungi mkono sera ya Marekani ya kuweka shinikizo kali dhidi ya Tehran.
Mpango huo hatahivyo utaiga ule wa majeshi yanayoongozwa na Marekani.
Badala ya kukabiliana na ugaidi pamoja na biashara haramu ya mihadarati, ujumbe huo mpya utakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa kuna uhuru wa uchukuzi katika mkondo huo wa bahari miongoni mwa meli za kimataifa kulingana na wizara hiyo ya Uingereza.
Ujumbe huo utabuniwa haraka iwezekanavyo, lakini kwa sasa meli ya kijeshi ya HMS Duncan imetumwa ili kuimarisha usalama wa meli za Uingereza na wafanyakazi wake katika eneo hilo, bwana Hunt aliambia wabunge hao.
Bwana Hunt alisema kuwa Uingereza iliamua kutochochea zaidi mgogoro huo lakini kwamba haitajali kuhakikisha kuwa kuna uhuru wa meli kupita katika mkondo huo bila wasiwasi.
Uchanganuzi wa Jonathan Marcus
Uingereza inahitaji usaidizi katika eneo la Ghuba kuhakikisha kuna usalama wa meli zake za kibiashara.
Juhudi za pamoja na mataifa mengine hazitaleta meli zaidi pekee bali pia zitapunguza mgogoro wa kibiashara kati ya London na Tehran.
Na kwa usawa. Kufuatia wasiwasi uliopo, kuna hatari kubwa ya meli za kibiashara zinazopitia mkondo huo wa Hormuz.
Jeshi la majini lililopendekezwa na Ulaya pia lina faida ya kutoongozwa na Marekani.
Utawala wa rais Trump umekuwa na mipango yake ya kubuni jeshi la majini kwa wiki kadhaa sasa.
Mataifa hayataki kuonekana yakijiunga na jeshi hilo katika kile kitakachoonekana kuwa muungano dhidi ya Iran.
Hatahivyo kulingana na wizara ya maswala ya kigeni nchini Uingereza kutakuwa na haja ya kuona kwamba juhudi hizo za Ulaya zinaunga mkono pandekezo hilo la Marekani. Washhngton ina ujasusi na uchunguzi wa hali ya juu ambao utahitajika.
Hilo hatahivyo litasalia kuwa wazo badala ya mpango wa kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment