Adbox

Tuesday, July 23, 2019

Yanga SC watoa kipigo cha goli 7-0


Yanga SC imeshinda mechi ya tatu mfululizo leo katika kambi yake ya Morogoro kujiandaa na msimu upya baada ya kuichapa ATN 7-0 Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro.

Pia Yanga SC inajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa Agosti 4, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Mwananchi dhidi ya timu ambayo itatajwa baadaye kufuatia kujitoa kwa AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana amefunga mabao matatu peke yake, huku mengine mawili yakifungwa na nyota wa Namibia, Sadney Urikhob, Mganda Juma Balinya na beki Mghana, Lamine Moro moja kila mmoja. 

Mechi mbili zilizotangulia Yanga ilishinda 2-0 dhidi ya Moro Kids mabao ya Balinya na beki wa kulia, Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye alikosekana leo kufuatia kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania kwa maandalizi ya mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Kenya Jumapili.

Na mechi ya kwanza Yanga ilishinda 10-0, kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa akifunga mabao matatu peke yake, mengine Feisal Salum, Raphael Daudi, Mapinduzi Balama, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, Wanyarwanda Patrick Sibomana, Issa Bigirimana na Balinya

No comments:

Post a Comment

Adbox