Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imelaani vikali waraka wa Makatibu Wakuu wastaafu wa chama hicho, Abdulrahaman Kinana na Yusuph Makamba walioutoa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni bila ya kufuata Kanuni na taratibu zilizopo.
Akiwasilisha tamko hilo leo jijini Dodoma Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa Henry Msunga amesema kitendo hicho cha kumhusisha mwanaharakati Cypria Musiba na CCM ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na miiko ya chama.
Amesema matamko yaliyotolewa na Musiba ni ya binafsi na hivyo ilipaswa viongozi hao wastaafu kushughulika na mtu binafsi na sio taasisi.
“kitendo cha kumuhusisha mwanaharakati cypriani musiba na chama chama cha mapinduzi ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na miiko yay a chama hasa ikizingatiwa kwamba matamko yaliyotolewa ni ya binafsi hivyo ilipaswa viongozi hawa washughulike na mtu na sio chama”alisema
Mbali na hayo amesema halmashauri Kuu ya CCM mkoa inaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kazi nzuri inayoifanya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa ndugu Godwin Mkanwa amesema CCM mkoa wa Dodoma ipo imara na imejipanga kuhakikisha inatetea haki za wanyonge.
“sisi tupo tayari kushirikiana na mh raisi kwa kazi nzuri anazozifanya za kutetea haki za wanyonge na kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 kila mkazi wa Dodoma anakua na makazi mazuri hiyo inaonyesha jinsi gani chama kinafanya kazi”alisema Mkanwa
No comments:
Post a Comment