Adbox

Tuesday, July 23, 2019

Sauti zinazodaiwa kuwa za Nape, Kinana na Membe kuchunguzwa


Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema sauti zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikihusisha sauti zinazofanana na baadhi ya makada wa CCM ni tukio la jinai, polisi wanaendelea na uchunguzi.

Akizungumza suala hilo, Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala alisema kwamba hiyo ni jinai na wenye mamlaka ya kuchunguza jinai ni Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo inakuja mara baada Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kusema bado wanachunguza ili kubaini ukweli na hakuna jambo kama hilo linaweza kupita wasilichunguze.

Ikumbukwe sauti hizo fupi za mazungumzo ya simu zinadaiwa kuwa za Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye; aliyekuwa waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), January Makamba; makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba pamoja na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Benard Membe.

No comments:

Post a Comment

Adbox