Korea Kusini ilirusha makombora ya kuionya ndege ya kijeshi ya Urusi


Ndege za kijeshi za Korea kusini aina ya F-15K zilitumwa kuizuia ndege hiyo ya UrusiHaki miliki ya pichamapigo.com
Image captionNdege za kijeshi za Korea kusini aina ya F-15K zilitumwa kuizuia ndege hiyo ya Urusi

South Korea ilirusha makombora ya kuionya ndege ya kijeshi ya Urusi aina ya A-50 ilipoingia katika anga yake siku ya Jumanne, Wizara ya ulinzi imethibitisha.
Maafisa wanasema kuwa ndege hiyo ya Urusi ilikiuka anga yake katika eneo la Dokdo/Visiwa vya Takeshima ambavyo vinamilikiwa na Seoul lakini pia Japan inadai kuwa katika himaya yake.
Waziri wa ulinzi nchini Korea Kusini alisema kuwa ndege zake ziliifuata ndege hiyo na kuirushia makombora ya kuionya.
Makombora zaidi yalirushwa baada ya ndege hiyo kurudi tena katika anga ya Korea Kusini.
Hiki ni kisa cha kwanza kutokea kati ya Urusi na Korea Kusini.
Moscow imekana kwamba ndege yake ya kijeshi iliingia katika anga ya Korea kinyume na sheria.

Ni nini ambacho Korea Kusini inasema kilifanyika?


Ramani ya Korea Kusini na Japan

Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa ndege hiyo ilikuwa mojawapo ya ndege tatu za Urusi na mbili za jeshi la China ambazo ziliingia katika anga ya KADIZ , ambapo ndege za mataifa mengine ni sharti zijitambulishe mapema siku ya Jumanne.
Ndege za kijeshi za Urusi na China zimekuwa zikiingia katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni.
Hatahivyo Korea Kusini inasema kuwa moja ya ndege hizo ilipaa zaidi na kuingia katika anga ya nchi hiyo mwendo wa saa tatu alfajiri saa ya Korea.
Ndege za Kijeshi za Korea Kusini F-15k na F-16k zilitumwa kwenda kuizuia.
Mkuu wa kitengo cha usalama nchini Korea Kusini Chung Eui-yong amewasilisha malalamishi kwa baraza la usalama la Urusi na kulitaka kuchukua hatua kali.
''Tunakichukulia kitendo hiki kama kisichokuwa cha kawaida , na iwapo kitarejelewa tutachukua hatua kali, afisi ya rais wa taifa hilo ilimnukuu bwana Chung akisema. Hakujakuwa na tamko lolote kutoka China