Naibu Waziri Mkuu Denys Shmygal anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Honcharuk. Shmygal awali alihudumu kama mkuu wa utawala wa kikanda katika jimbo la magharibi la Ivano-Frankvisk kabla ya kuchukua wadhifa wa naibu waziri mkuu mwezi uliopita.
Hakukuwa na kauli ya mara moja kutoka kwa Honcharuk au Rais Volodymyr Zelenskiy. Haijafahamika wazi kilichomfanya Honcharuk kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa mara ya pili.


No comments:
Post a Comment