Na Paschal D.Lucas, Mwanza
Shirika la Cassava Plantatiob and AgriBusiness Foundation (CAPAFO) Nchini Tanzania limekuja na mkakati mpya wa kuwainua wakulima wadogo wadogo wa Alizeti na mihogo ili kuogeza thamani na tija katika kilimo na uvunaji wa mazao hayo.
Akifungua Semina ya jinsi Uvunaji na utunzaji wa Alizeti Katika vikundi vya vya wakulima katika kijiji cha Sima Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Mwenyekiti wa CAPAFO Mkoani humo Bw.DENIS NYAMLEKELA amewataka wakulima waache njia waliyoizoea kulima, kuvuna na kuhifadhi bali watumie mafundisho na semina watakayofundishwa na Mtaalamu wa Kilimo cha Alizeti kutoka Nchini Marekani Bi GRET(Pichani aliyesimama) ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Kwa upande wake Bi.JOSEPHINE KAPOMA kutoa shirika USAID IAC Farmer to Farmer Mkoani Morogoro amesema ametimiza ahadi aliyowaahidi wanachama wa vikundi hivyo kuwa atawaletea mgeni na mtaalamu wa kilimo cha Alizeti hususan uvunaji na utunzaji na kuwaeleza kuwa Mtaalamu huyo atakuwepo kwa siku nne hivyo watumie fursa hiyo kujifunza na kuelewa ipasavyo kuhusu zao la alizeti.
Aidha Bi.Kapoma ameongeza kuwa kwa kuwa wanavikundi hao wamefanya semina na mafunzo hayo hivyo wajitahidi kuwa wasikivu kwani kadri wanavyozidi kupata mafunzo hayo ndivyo wanavyoongeza maarifa na kutambua kuwa wapi walikosea wakati wanafanya kilimo hicho na kuongeza upeo wa kutambua zao hilo.
Bi.GRET atakuwepo Sima Sengerema kwa siku nne hivyo ataendelea kutoa semina hiyo mpaka March 7,2020.



No comments:
Post a Comment