Adbox

Wednesday, March 4, 2020

Libya yahamisha safari za ndege kutoka uwanja wa Mitiga, Tripoli

Maafisa katika uwanja pekee unaofanya kazi katika mji mkuu wa Libya Tripoli wamesema jana usiku kuwa wanahamisha safari zote hadi mji wa Misrata kutokana na mashambulizi katika eneo hilo kufuatia kuongezeka kwa mapigano katika siku za karibuni.

 Uwanja wa ndege wa Mitiga umefungwa mara kadhaa katika siku za karibuni kutokana na mashambulizi ya maroketi na safari za ndege hapo jana ziliahirishwa kwa sehemu kubwa.

Mashambulizi ya maroketi kuelekea uwanja huo yameongeza katika mwishoni mwa wiki iliyopita wakati juhudi za Umoja wa Mataifa kuzileta pamoja pande zinazozana mjini Geneva zikishindwa kufua dafu.

Jumatatu wiki hii, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Ghassan Salame alitangaza kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment

Adbox