Waandishi wa habari 18 wameshiriki mafunzo ya warsha ya kuvuna matokeo kati ya waandishi wa habari 48 walioshiriki mafunzo hapo 2019 juu ya wanawake na uongozi ikiwemo Siasa yaliyoandaliwa na shirika la TGNP Mtandao kwa kushirikiana na UN-Women ambayo yaliyoshirikisha mikoa mitano iliyopo nje ya Dar-es salamu.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali TGNP Mtandao,Liliani Liundi leo amewaambia waandishi hao kuwa lengo la warsha hiyo ni kujenga na kuongeza uwelewa na uwezo kwa waandishi wa habari ili kuripoti maswala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na Vijana kwenye uongozi.
"Kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti maswala ya kijinsia katika vyombo vya habari hasa kusambaza ilani ya uchaguzi ya wanawake na kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi ni mda wa wanawake kuacha tabia ya kubebwa badala yake wajisimamie"alisema Liundi.
Kwa upande wake Monica John ambaye ni Afisa habari wa shirika la TGNP alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuandika habari za kijinsia hasa zenye kuhamasisha mila desturi na mitazamo chanya inayo hamasisha jamii kuwachagua na kuwahamasisha wanawake kushiriki katika uongozi ili kuweza kuongeza idadi ya wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi ikiwemo ya kisiasa.
Monica aliongeza kuwa shirika linategemea kuona waandishi wa habari wanasaidia kufanya vizuri kwa kutumia kalamu zao katika kuandika habari za kuinua kundi la wanawake na vijana katika jamii hususani kwenye maswala ya kugombea uongozi bila kuathiri pande zote.
Mmoja wa washiri wa semina hiyo kutoka mkoani Mara Frankius Cleophace alisema kuwa swala la kuwainua wanawake juu ya maswala ya kugombea nafasi za uongozi ni endelevu kwasababu jamii inakuwa kila siku na inahitaji swala mtambuka kuwadhamini wanawake na vijana katika kuwainua na kuwahamasisha juu ya kugombea nafasi za uongozi.
"Sisi kama waandishi wa habari ambao tayari tumeaminiwa na jamii sasa ni jukumu letu kuendelea kupaza sauti ili wanawake wajitokeze kwa wingi kwa lengo la kuwani nafasai za uongozi alisema Frankius



No comments:
Post a Comment