Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imejipanga kuboresha majosho ya kuogeshea mifugo na kujenga mengine mapya ikishirikiana na wafugaji ili kupambana na magonjwa mbalimbali ambayo sababishwa na kupe ambayo yamekithiri kwa kiasi kikubwa mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi John Palingo akifungua Josho la kuogeshea Mifugo lililokarabatiwa kwa nguvu za wafugaji katika Kijiji cha Songwe Kata ya Nanyala wilayani humo alisema Halmashauri yake imejipanga kuboresha majosho yote ambayo yalisha haribika kutokana na usimamizi mbaya uliopelekea mengi kuharbika na kusababisha Mifugo mingi kukumbwa na magonjwa yasabishwayo na kupe.
Alisema Halmashauri ya Mbozi ilikuwa na majosho 20 awali lakini mpaka sasa majosho ambayo yanaweza kukarabatiwa ni majosho nane ambapo tayari wameanza na Josho la Songwe ambalo litatumika kuogesha mifugo 5946 kutoka kata ya Nanyala na vijiji jirani.
"Tutaboresha majosho nane na kujenga mengine mapya ili kutatua kabisa magonjwa yanayosababishwa na magonjwa yatokanyo na kupe ambayo kwa kiasi kikubwa hupelekea mifugo mingi hasa ng'ombe kudhoofika na mingine kufa kabisa,
Kukamilika kwa josho hili kunatutaka wafugaji wote kuogesha mifugo kwa kuchangia kiasi cha shilingi 200 kwa kila mfugo kama mlivyokubaliana na viongozi wenu, Wizara ya Mifugo imetoa mwongozo kuwa mfugaji atakaye kiuka kuogesha Mifugo atachukuliwa hatua , siyo hiari tena kuogesha Mifugo yenu , kwa wale watakaokiuka watalazimika kulipa faini kuanzia shilingi laki tatu mpaka laki sita au miezi mitano jela , lengo la Wizara ni kuwataka wote muogeshe mifugo yenu ili muweze kuwa na mifugo yenye afya itakayo wanufaisha ninyi wafugaji ili kuondokana na umasikini " alisema Palingo.
Kwa upande wake Afisa Mifugo na uvuvi wilayani Mbozi Danford Mwelelwa alisemema wamejipanga kukamilisha majosho mengine nane kufikia msimu wa kiangazi ili kukomesha kabisa magonjwa yanayosababishwa na kupe .
Alisema asilimia 72 ya magonjwa ya Ng'ombe husababishwa na kupe hivyo utengenezwaji wa majosho waliouanzisha utapelekekea kutatua asilimia kubwa ya magonjwa na kupunguza vifo vya mifugo vilivyo kuwa vinatokea kila mwaka , aliongeza kuwa Ng'ombe zaidi ya 55 walikuwa wanalipotiwa kufa ndani ya wilaya ya Mbozi kila mwaka kutokana na kukosekana Kwa majosho ya kuogeshea mifugo hivyo Mifugo kukumbwa na kupe wengi ambao ndio kisababishi kikubwa cha magonjwa.
Aliyataja baadhi ya magonjwa ambayo husababishwa na kupe kwa Mifugo kuwa ni ndigana kali, ndigana barid na ugonnjwa wa moyo ambapo huibuka zaidi kipindi cha masika kunapokuwa na mvua nyingi .
"Serikali kupitia wizara ya Mifugo na uvuvi tayari imeshatoa dawa kwa ajili ya kupambana na kupe kwa wafugaji, hivyo sisi tunaboresha haraka majosho na kujenga mapya tukishirikiana na wafugaji baada ya kuwapatia elimu namna ya kunusuru Mifugo yao kupata magonjwa yanayosababishwa na kupe "alisema Mwelelwa.
Mmoja wa Wafugaji Wilson Mwazembe alisema kukamilika kwa Josho hilo kutakuwa suluhisho ya Mifugo yao kufa ambapo walikuwa wanapata changamoto kubwa kutoka ya kununua dawa ambazo muda mwingine zilikuwa hazitibu magonjwa yanayoikumba Mifugo yao.
"Tunaishukuru Halmashauri yetu ya Mbozi kwa kutupa ushirikiano mkubwa na kupelekea kukamilika kwa Josho hili ambalo tumelililia kwa muda mrefu sana" alisema Mwazembe ambaye ni mfugaji.
Naye Gibson Adam alisema kuwa walikuwa wanatumia gharama kubwa kununua dawa kwa ajili ya kupulizia Mifugo yao , lakini kupitia josho walilokarabati wakishirikiana na Halmashauri kwa ukarbu litapunguza gharama na kupelekea Mifugo yao kuwa salama kabisa.


No comments:
Post a Comment