Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma mara baada ya kuwasilisha mada katika semina maalumu kwa Wanahabari kwa ajili ya kuwajengea uwezo kufahamu mashindano hayo, kwa wanahabari.
Mkurugenzi idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Maulilio Kipanyula amesema mashindano hayo yanalenga kutambua wabunifu kutoka kwenye makundi saba ya shule za msingi,shule za sekondari,vyuo vya ufundi stadi,vyuo vya kati.
Vyuo vikuu,taasisi za utafiti na maendeleo na wabunifu kutoka mfumo usio rasmi huku lengo kuu likiwa ni kuibua,kutambua na kuendeleza ubunifu.
Prof.Kipanyula amesema mashindano hayo yamekuwa na Manufaa makubwa kwani kutokana na mashindano hayo mwaka jana waliweza kuibuka washindi 60 ambapo wameendelezwa na kwa sasa wanajipatia kipato kutokana na ubunifu wao.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Sylvia Lupembe amesema kwa mwaka huu washiriki wabunifu waliojitokeza kushiriki mashindano hao ni 583 na zoezi lilishafungwa huku tathimini ikiendelea kufanyika.
Kwa upande wake Mtaalam wa Fizikia ya Mionzi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia,Edwin Konzo amesema hakuna ukomo wa ushiriki kwenye ubunifu isipokuwa mbunifu anatakiwa kuja na ubunifu mwingine maana ubunifu alioshiriki mwanzo utakuwa umeingizwa kwenye kanzi data[Data base]huku akibainisha kuwa uchoraji nao ni ubunifu .
Jumla ya Washindi 21 katika makundi 7 yataibuka katika Mashindano hayo ambapo Mshindi wa kwanza atapewa tuzo ya Tsh.milioni tano[5000,000],Mshindi wa pili milioni tatu[3000,000] ,mshindi wa tatu milioni mbili[2000,000].
Ikumbukwe kuwa Mashindano ya MAKISATU yalianza mwaka jana na mwaka huu uratibu wa Mashindano hayo ni Wyest&Ofisi ya Rais -TAMISEMI,tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia[COSTEC] Pamoja na VETA huku kaulimbiu ni “Sayansi,Teknolojia,na ubunifu kwa uchumi wa viwanda huku Taasisi 61 zikithibisha kushiriki katika mashindano hayo.




No comments:
Post a Comment