Adbox

Monday, March 2, 2020

Korea Kusini yaripoti maambukizi mapya 500 ya virusi vya corona

Korea Kusini imeripoti leo karibu visa vipya 500 vya virusi vya corona, ikiwa ni idadi kubwa kabisa ya kitaifa kushuhidiwa duniani nje ya China kupindukia 4,000.

Watu wanne zaidi wamefariki dunia, na kufikisha 22 idadi ya vifo nchini humo. China imeripoti visa vipya 202 vya maambukizi ya virusi hivyo na vifo 42 hapo jana, na kufikisha 80, 026 jumla ya idadi ya maambukizi China bara.

Jumla ya idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo ni 2,912 kwa mujibu wa Tume ya Kitaifa ya Afya. Zaidi ya nusu ya wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo tangu vilipozuka sasa wamepona, kwa mujibu wa habari rasmi.

Wakati takwimu zikionyesha kuwa ugonjwa huo umepungua kasi nchinji China, maambukizi katika maeneo mengine yanaongezeka.

Italia imeripoti kuongezeka maambukizi ya virusi hivyo kwa asilimia 50 na kufikia 1,694.

No comments:

Post a Comment

Adbox