Adbox

Monday, March 2, 2020

Waziri mkuu mteule wa Iraq ajiuzulu

Waziri mkuu mteule wa Iraq Mohammad Allawi amejiondoa katika jukumu la kuunda serikali, hatua ambayo inaitumbukiza nchi hiyo katika sintofahamu ya kisiasa, na kumuacha Rais Barham Saleh na siku 15 kupendekeza mgombea mpya, ambaye anaweza akamtaja moja kwa moja bila kushauriana na bunge.

Akiijibu taarifa ya kujiondoa Allawi, Saleh alisema ameanzisha mashauriano ya kumtangaza mtu mwingine katika muda uliowekwa na katiba.

Iraq imekuwa katika mkwamo wa kisiasa tangu waziri mkuu anayeondoka Adel Abdel Mahdi alipojiuzulu Desemba, kwa sababu katiba haina vifungu vya kushughulikia hatua ya aina hiyo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Allawi amesema alichukua hatua hiyo kwa sababu baadhi ya makundi ya kisasa hayakuwa makini kuhusu mageuzi, wala kuzitekeleza ahadi zao kwa watu.

Wakati hayo yakijiri, jeshi la Iraq limesema makombora mawili yalilipiga eneo la ubalozi wa Marekani pamoja na kituo cha wanajeshi wa Marekani mjini Baghdad.

No comments:

Post a Comment

Adbox