Adbox

Monday, March 23, 2020

Idadi ya maambukizi yafikia watu 8,961 Korea Kusini

Kwa takribani mwezi mmoja Korea Kusini leo hii imeripoti kiwango cha chini cha ongezeko la visa vipya vya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa kituo cha udhibiti magonjwa na kinga cha nchi hiyo (KCDC) kumerekodiwa maambukizi mapya 64, ikiwa ongezeko dogo tangu Februari 25, na kufanya idadi jumla ya maambukizi hayo kufikia watu 8,961.

Watu saba wengine ambao walifanyiwa vipimo vya ugonjwa wa COVID19 wamekufa na kufanya jumla ya vifo nchini humo kufikia 111.

Idadi kubwa ya waliokufa walikuwa wazee, ambao pia walikuwa na magonjwa mengine nyemelezi.

No comments:

Post a Comment

Adbox