Mkuu wa shirika hilo, Alain Krakovitch amesema madaktari, wauguzi na maafisa wengine katika sekta ya afya wataweza kusafiri bure, katika kushiriki jitihada za kukabiliana na janga la virusi vya corona, lakini wakipata ridhaa ya viongozi wao.
Tangazo hilo linatololewa baada ya idadi ya waliokufa kutokana na virusi hivyo kufikia 674, na ikimjumuisha daktari wa kwanza aliyekuwa akishiriki mapambano ya kukabilina na mripuko wa virusi.
Tayari hospitali nchini Ufaransa zimeripotiwa kuwa na visa 7,240, na jeshi limeingilia kati kusafirisha wagonjwa kutoka katika miji iliyoathiriwa zaidi, na kuanzisha vituo vingine vya tiba katika maeneo mengine.


No comments:
Post a Comment