Adbox

Thursday, March 12, 2020

DPP kumchukulia hatua Lema

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema watamchukulia hatua Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kwa kitendo chake cha kusambaza taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Lema anadaiwa kutoa taarifa hizo hilo Februari 2020 wakati akizungumza katika mazishi ya katibu wa Chadema jimbo la Singida Mashariki, Alex Joas ambaye mwili wake ulikutwa kando ya barabara ukiwa na majeraha kichwani.

Machi 2, 2020 mbunge huyo ambaye pia mjumbe wa kamati kuu Chadema alikamatwa na polisi jijini Arusha na kusafirishwa usiku hadi Singida kwa hatua zaidi, baadaye aliachiwa kwa dhamana

Leo Alhamisi Machi 12, 2020  Mganga amewaambia wanahabari kuwa watamchukulia hatua mbunge huyo ingawa hakuweka wazi hatua gani, akisisitiza anazifahamu yeye mwenyewe.

‘Hatua nitakazozichukua nazifahamu mimi na ofisi, mtaziona wakati nitakapozichukua kwa sababu hazitafanyika kwa kificho kama nitamshtaki au la nitaangalia," amesema Mganga.

Katika maelezo yake, Mganga amesema taarifa zilizotolewa za mbunge huyo si kweli akisema amepitia jalada moja baada ya nyingine na kubaini polisi wamezifanyia kazi taarifa hizo tofauti na maelezo ya Lema.

No comments:

Post a Comment

Adbox