Kupitia mtandao wa Twitter, rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel amesema chochote kinachoweza kuvuruga uchumi kinapaswa kuepukwa.
Michel amesema Umoja wa Ulaya unafanya kila juhudi kuzuia kuenea kwa homa ya virusi vya corona, ijulikanayo kama COVID-19, na unasaidia katika utafiti juu ya kirusi hicho.
Marufuku ya usafiri iliyotangazwa na Rais Trump itawahusu watu wote wasio raia wala wakazi wa nchini Marekani, lakini Ikulu ya Marekani, White House imesema haijumuishi bidhaa.


No comments:
Post a Comment