Adbox

Wednesday, March 25, 2020

Congo yafunga mipaka na kutangaza hali ya dharura

Rais wa Jamhuri ya kideomkrasia ya Congo Felix Tshisekedi, jana ameamrisha kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo na kutangaza hali ya dharura ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona hatua iliyochukuliwa na mataifa mengine ya bara Afrika katika siku za hivi karibuni kuimarisha udhibiti wa virusi hivyo.

Virusi hivyo vinaenea kwa kasi barani Afrika na kufikia sasa watu 1700 wamepata maambukizi katika mataifa 45 barani humo.

Zaidi ya watu 40 nchini Congo wamepata maambukizi huku watatu wakifariki na kuibua hofu ya kusambaa kwa virusi hivyo hasa katika mji mkuu wa Kinshasa ulio na idadi kubwa ya watu.

Katika hotuba yake kwa taifa hapo jana, rais Tshisekedi alisema kuwa virusi hivyo havihitaji paspoti ama kadi ya kura kuenea majumbani na kwamba watu wanajipata katika vita na adui asiyeonekana.

No comments:

Post a Comment

Adbox