Adbox

Wednesday, March 25, 2020

Xi Jinping kushiriki mkutano wa G20 kwa njia ya video

Shirika la habari la serikali nchini China , limeripoti leo kuwa rais wa nchi hiyo Xi Jinping atashiriki katika mkutano wa viongozi wa mataifa 20 yalioendelea na yanayoinukia kiuchumi G20 utakaondaliwa siku ya Alhamisi kupitia video.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo, mfalme wa Saudi Arabia Salman, ataongoza mkutano huo utakaoangazia juhudi za pamoja za kimataifa za kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona.

No comments:

Post a Comment

Adbox