“Nashukuru kwa kunikaribisha, nimefurahi kuwa nanyi, ila tufanye kazi kwa mashauriano kwa pamoja, ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali ambazo kila Wizara wanazo, na pia nasi tunazo, “ alisema Kadio.
Pia Kadio alielekeza kuonana na kila Mkuu wa Idara na Kitengo baada ya makabidhiano hayo, ili kusikiliza majukumu yao, pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kutafuta njia ya kuzitafua.
“Nataka mje tuzungumza, kila mmoja wenu aje ofisini kwangu tuzungumze, na pia muwe wazi, muwe wakweli ili nijue majukumu yenu, changamoto zenu ili tuweze kusaidiana,” alisema Kadio.
Katibu Mkuu Kadio pia aliwapongeza kwa kazi nzuri ambazo Wizara imekuwa inazifanya kwa kipindi chote na kupitia utendaji huo mzuri kuna maboresho na mafanikio ya mambo mbalimbali ndani ya Wizara.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya licha ya kuwepo kwa changamoto lakini tutapambana nazo, kuna maboresho na mmefanikiwa mambo mengi na bado tuna fursa ya kufanya mazuri zaidi,” alisema Kadio.
Pia Kadio alisema anapenda kila kiongozi kuwa wazi, na kusema yoyote bila woga kwasababu anataka ukweli katika utendaji wake wa kazi.

No comments:
Post a Comment