Agizo hilo limetolewa na katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Lindi Innocent Nanzaba baada ya wakulima 139 kufika kufika ofisi za chama kuomba msaada kwa chama hicho kiingilie kati mgogoro huo ambao unaweza kuvuruga amani kwa wakazi wa kijiji hicho
Nanzaba Alisema amepokea ujumbe wa wakulima 139 ambapo umewakilishwa na wakulima 13 kutoka kijiji cha Mnengula kata ya Mnolela wamelalamikia watendaji na uongozi wa Manispaa ya Lindi kugawa eneo lao kwa mwekezaji na kukwamisha shughuli za wakulima hao kuendekea na kilimo.
Alisema CCM inatambua kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya watendaji wasio waadilifu na waaminifu ambao wanatumia ofisi zao kuni
jinufahmisha bila kukumbuka kuwa wao ni wasaidizi wa Rais wa kutatua kero za wananchi
"Tumepokea malalamiko ya wakulima kuhusu mgogoro wao na mwekezaji CCM itatembea eneo hilo na kulifanyia kazi ili kutatua huo mgogoro maana sisi tumekuja kumsaidia Rais wetu ambae ndie Mwenyekiti wa Chama kazi,na hatupendi kuona wananchi wanapeleka lalamiko yao wakati wa ziara za viongizi wa juu akiwemo rais kwa mabango nawaomba watendaji kuumaliza mgogo huo kwa muda wa siku saba baada ya hapo chama kitachukua uamuzi"alisema Nanzaba
Alisema cha mapinduzi hakitakubali kuona wananchi wanyonge wakinyanyaswa na kubuguziwa na watu wachache kwa maslahi binafsi kwa madai ya kuwa wao ni wawekezaji ,CCM inatambua umuhimu wa wawekezaji lakini kwa wale wanaotambua utu wa wao na kufuata utaratibu uliwekwa.
Salumu Nanokori Alisema watendaji wa serikali ya wilaya imeonekana wanamaslai na mwekezaji kwani wameamua kufumbia macho suala la mgogoro huo hali iliyosasabisha wananchi kukiomba chama cha mapinduzi kuingilia kati kwa lengo la kutatua mgogoro huo ili wananchi waendelee na uzalishaji kwa kuendelea kuendesha kazi yao ya kilimo ili kuwafanya waweza kuepuka na balaa la njaa.
Ili tatizo linashindwa kutatuliwa inaonyesha kuna baadhi ya watendaji wananufaika ndiyo maana wananchi tunatishwa na tutakamatwa na polisi tunawekwa ndani bila sababu aluekeza Salumu.
Alisema kuwa eneo hilo la zaidi ya hekari 350 Manispaa ya Lindi imempa mwekezaji wakati wakulima wa kijiji cha Mningula jimbo la Mtama walikuwa wanaendesha shughuli za kilimo kwa muda mrefu
Katibu mwenezi CCM kata ya Mnolela Juma Bakari alisema kuwa wananchi wa eneo hilo wameteseka kwa muda mrefu ikiwemo kukamatwa na polisi na kuwekwa rumande bila ya ufumbuzi wa suala hilo , mpaka wanalifikisha Ccm ngazi zingine wameshiindwa kulitafutia ufunbuzi wa kudumu
Bakari alisema kuwa baada ya kukosa suluhisho la mgogoro kwenye ngazi ya watendaji akiwa na pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Lindi wakulima hao wameamua walikwenda ofisini kwake nakuomba msaada wa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao wa muda mrefu ulisababisha baadhi ya wananchi kusimamisha shughuli zao za kilimo ndipo alipowafikisha ccm mkoa kutoa malalamiko yao.
Zainabu Saidi ambae ni miongoni mwa wananchi waliko kwenye mgogoro huo alisema wamemuomba katibu huyo wa CCM mkoa kutatua mgogoro huo ambao umeonekana kudumu kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu wakishindwa kufanya shughuli za kilimo.
Zainabu alisema mgogoro umesababisha wananchi kushindwa kufanya kazi za kilimo kwenye eneo hilo pia umekuwa ukiwanyima amani kwani mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa ndani kwa madai wanaendesha shughuli za kilimo kwenye eneo la mwekezaji.


No comments:
Post a Comment