Adbox

Saturday, January 4, 2020

Wasajili laini kwa alama za vidole watuhumiwa kuwaibia wateja wao pesa kwenye akaunti

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limebaini ongezeko la matukio ya utapeli unaohusisha usajili wa laini za simu baada ya Rais John Magufuli kuongeza siku 20 za usajili  baada ya kundi la vijana linalovalia vikoti vya kampuni za mawasiliano kutembelea wateja majumbani.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Nyamagana (Jiji), Juma Jumanne alisema takwimu zinaonyesha kuanzia Januari hadi Novemba, 2010 matukio ya utapeli juu ya usajili wa simu yakuwa saba tu lakini ghafla yamepanda Desemba mwaka jana.

Alisema kuwa mwezi huu wa Januari mwaka huu, ambayo bado mwezi mchanga wamepokea matukio ya wizi wa pesa yanayofanywa na kundi hilo hilo, yupo mkazi aliyetapeliwa na kutioa namba ya sii ya benki na kuibiwa Sh milioni 4, mwingine Sh  900,000 na Shilingi milioni mbili.

"Tumepokea matukio ya mawakala ambao wanafanya miamala ambao nao wameibiwa simu wanazofanyia miamala ya pesa ambazo zimeibwa, yaani kuna mteja anaiba simu kituo fulani anatoa fedha zote kisha anaiacha kituo kingine na kuchukua nyingine yenye pesa," alisema.

No comments:

Post a Comment

Adbox