Kamanda wa Polisi mkoani humo Hamis Issah, amesema kuwa tukio hilo limesababishwa na uwepo wa ugomvi wa kifamilia na imani za kishirikina, uliopelekea kutoelewana kati ya baba na mtoto, ambapo mara baada ya mzee huyo kujeruhiwa, alipelekwa hospitali na baadaye kufariki baada ya hali yake kuwa mbaya.
"Kuna mzee mmoja ameuwawa ana umri wa miaka 72, kutokana na kuwepo kwa ugomvi wa kifamilia ulioleta hali ya kutoelewana, kutokana na mtoto mmoja kwenye familia hiyo kugombana na baba yake na kuchukua kitu chenye ncha kali na kumjeruhi mzee wao" amesema Kamanda Issah.
Aidha katika hatua nyingine Kamanda Issa amesema kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, zimesababisha watoto wanne kufariki dunia katika nyakati na maeneo tofauti ya Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment