Adbox

Monday, January 6, 2020

Vifaa vya NIDA vyaibwa na watu wasiojulikana

Vifaa vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), katika ofisi za NIDA zilizopo maeneo ya Arusha DC, wilayani Arumeru vimeibiwa na watu wasiojulikana.   

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Polisi, wilayani Arumeru, Kamanda Mapunda, kupitia kwa Afisa Habari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Abel Stanford, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililotokea usiku wa kuamkia leo Januari 6, 2020.

"Ni kweli kwamba kuna uvunjifu umefanyika maeneo ya Ofisi za NIDA hapo Arusha DC, wameiba Camera 2, Desktop 1, Laptop 2, ila Mratibu wa Polisi Arumeru yuko eneo la tukio anafuatilia, baadaye tutatoa taarifa kamili" amesema Abel.

No comments:

Post a Comment

Adbox