Shirika la msaada wa kisheria na haki za binadamu wilayani Newala ( PCO) limevuka lengo liliojewekea la kufikisha elimu ya kisheria kwa watu 24, 000, mwaka 2019 hadi 2020.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa shirika hilo, Bakiry Mtanda, jana wakati anazungumza na Muungwana Blog kwenye ofisi ya shirika hilo lililopo mjini Newala.
Mtanda alisema lengo la shirika hilo lilikuwa ni kufikisha elimu ya kisheria kwa watu 24,000 hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu (2020) hata hivyo limeweza kuwafikia watu hao na zaidi, kabla ya muda huo kutimia.
Alisema kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2019 walikuwa wamefikisha elimu kwa watu 20,987. Hata hivyo kwa robo iliyotangulia ambayo ilianza mwezi Julai mwaka huo na utekelezaji wake kuanza mwezi Agosti waliweza kufikisha elimu kwa watu 3,326.
Mtanda alisema mbali na kufikisha elimu, lakini pia kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2019 walitoa usaidizi wa kisheria kwa watu 24. Lakini kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba walitoa usaidizi kwa watu 123.
" Sababu yakuwa na idadi ndogo ya tuliowasaidia ni pamoja na jamii hasa iliyopata elimu kuanza kutambua haki zake, wajibu na sheria. Lakini pia baadhi ya watu hawajui kama mambo wanayofanya na kufanyiwa ni ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu. Kwahiyo hao hawaji kulalamika na kuomba msaada wa kisheria," alisema Mtanda.
Hata hivyo mkurugenzi huyo wa PCO alisema kuanzia mwezi huu wa Januari shirika hilo linatarajia kupokea watu wengi, hasa wanawake ambao watahitaji msaada wa kisheria. Kutokana na ndoa nyingi kuvunjika na kusababisha ukatili wa kijinsia.
Alisema wilayani humo msimu wa ununuzi na uuzaji wa korosho wanawake wengi wanapewa talaka. Nikutokana na baadhi ya wanaume kutaka kuoa wanawake wengine, ili wasihojiwe na wake zao wakati wakupanga matumizi na kutumia fedha zilizotokana na mauzo ya zao hilo.
" Kwahiyo baada ya kumalizika msimu, watu watakuwa hawana fedha. Wakati huo shule zitakuwa zinafunguliwa wakati watoto wapo kwa mama zao ambao wameachwa na baba zao. Na wanawake hao wanakuwa hawana uwezo wa kumudu mahitaji ya shule. Ndipo mgogoro unaanza," alisema Mtanda.
Kiongozi huyo wa PCO alieleza sababu nyingine ya migogoro kuanza mwezi huo ni baadhi ya wanaume kwenda nje ya wilaya na mkoa wa Mtwara, hasa mkoa wa Lindi katika wilaya za Liwale na Ruangwa kulima mashamba ya ufuta, na kuwaacha watoto wakiwa na wake zao ambao wanashindwa kumudu gharama na mahitaji ya shule.
Saturday, January 4, 2020
Shirika la msaada wa kisheria Newala lavuka lengo la kufikisha elimu kwa jamii
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment