Adbox

Saturday, January 4, 2020

RPC Mbeya: Mwanamke aliyekutwa na watoto wawili waliopotea Mbeya si mgonjwa wa akili

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi  Ulrich Matei  amesema kuwa mwanamke aliyewachukua watoto wawili mkoani Mbeya Hawa Ally maarufu kama 'mkalipa' (40) mkazi wa Tegeta Jijini Dar es Salaam si mgonjwa wa akili.

Watoto hao wawili ambao ni Tarhana Mashaka Juma (mwaka 1) na Faisal Mashaka Juma (miaka 5) waliopotea mkoani Mbeya wamepatikana Tabora.

No comments:

Post a Comment

Adbox