Adbox

Wednesday, January 1, 2020

CCM kuandaa sera, ilani ya uchaguzi 2020 / 25

Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimesema kiko katika mchakato wa kuandika mwelekeo wa sera za CCM kwa mwaka 2020 hadi 2030 pamoja na uandaaji wa Ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020/2025.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Desemba 31, 2019 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema katika michakato yote ya uandaaji nyaraka muhimu za chama ikiwamo mwelekeo wa sera na Ilani huwa ni ushiriki na ushikishaji wa umma wa Watanzania na wanachama wa CCM kote nchini.

Amesema msingi huu wa kushirikisha umma unatokana na asili ya chama ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ni vitu viwili, kutenda haki na kuheshimu watu.

“Chama kinawakaribisha mtu mmoja mmoja au vikundi vya watu na taasisi mbalimbali ikiwamo lakini si kwa uchache, vyama vya wafanyakazi, wawakilishi na vyama vya wakulima, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, vyama vya waalimu, wachimbaji wadogo wadogo wa madini,” amesema Polepole

Vingine ni, wafanyabiashara wa madini, wawakilishi na vyama vya wakulima, wavuvi na wafugaji, jumuia za wamachinga na wasafirishaji wadogo wadogo, bodaboda na bajaj.

Polepole amesema jumuia za wanawake, watu wenye ulemavu, vijana, wazee, watoto, Asasi Zisizokuwa za Kiserikali (AZISE), wasomi, wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu, wadau na wana tasnia ya sanaa, burudani na michezo, wasafirishaji wa mizigo na abiria, wenye viwanda, wadau wa sekta ya utalii na vyama vya ushirika kwa maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

Adbox