MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) unatumia kiasi cha shilingi bilioni 5 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji unaojengwa mwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja, akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo, akiwa na mwemyeji wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiambatana na Mbunge wa Viti Maalum Zaynab Vulu.
Luhemeja alisema kuwa mradi huo mkubwa unaotekelezwa kwa fedha za ndani kutokana na makusanyo ya bili za wateja wake, ni utekeelezani wa dhamira ya serikali inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli.
"Kipekee kabisa niishukuru serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Magufuli, jana (juzi) tumezindua mradi mwingine mkubwa wa maji pale Kisarawe, maji yanayotokea katika chanzo cha Mto Ruvu yanayokwenda kupunguza kama.so kumaliza changamoto hiyo,"alisema Mhandisi Luhemeja.
Kwa upande wake Waziri Jafo alilipongeza shirika hilo kwa ufanisi wake mkubwa katika kusambaza maji maeneo mbalimbali, huku akisema hatua hiyo inafuatia dhamira kubwa na njema ya Rais Magufuli ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo ya maji.
"Sote tu mashahidi, tangu serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu kipenzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, miradi mingi ya kimaendeleo imekuwa ikitekelezwa katika wilaya na mikoa mbalimbali, nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati ya moyo wangu," alisema Waziri Jafo.
Kwa upande wake Ulega nae hakusita kuishukuru serikali kwa hatua hiyo kubwa, huku akieleza kwamba mradi huo unaojengwa hospitalini hapo, mbali ya kutoa huduma eneo hilo, pia maji hayo yatavinufaisha vijiji mbalimbali.
"Nikuombe ndugu yangu Jafo utufikishie salamu zetu za shukrani kwa Rais wetu John Magufuli, hakika anatupenda sana wana-Mkuranga, leo tunashuhudia ujenzi huo mkubwa wa tenki la maji linalolenga kuondoa changamoto husika," alisema Ulega.
Mbunge wa Viti Maalumu Zaynab Vulu aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuyafikisha maji hospitalini hapo, huku akisema huduma ya maji pamoja na umuhimu kwa binadamu wote, lakini wanawake ni watumiaji wakibwa wa maji.
"Tunaishukuru serikali yetu kupitia DAWASCO kwa mradi huo mkubwa l ambao leo tunaushuhudia hapa, utakuwa mkombozi katika eneo hili la hospitali, pia kama tulivyoelezwa na Mkurugenzi Luhemeja kwamba maji haya yatafika mpaka maeneo ya vijiji vyetu," alisema Vulu.
No comments:
Post a Comment