Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mrisho Yassin wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkataba walioingia na ATCL wa kuhudumia ndege, abira na mizingo ya Shirika hilo itakayokuwa inatua katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere na kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro.
Yassin amesema Swissport kuanza kuhidumia ATCL ni fursa kubwa kwao hivyo watakikisha wanalisapoti Shirika hilo kwa kujipanga kikamilifu kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora ili kuleta mabadiriko chanya.
"Kazi hii tuliyopewa ni kubwa na kiukweli ATCL kwa sasa ni jina kubwa hivyo tunapaswa kuitendea haki fursa hii, wafanyakazi wenzangu tukiharibu kwa watu hawa itatubomoa na Mimi kama kiongozi sipendi jambo hilo litokee," amesema.
Hata hivyo alisema jumla ya watu 90 wamepata ajira katika kampuni hiyo baada ya kuingia mkataba huo kwa lengo la kuongeza nguvu na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watanzania.
"Kiukweli kampuni tumejipanga kuhakikisha kwamba tunaweza kuwahudumia ATCL na kukidhi mahitaji yao kulingana na mkataba tuliyoingia, niendelee kuwahakikishia kwamba hatuyawaangusha," amesema.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mipango ATCL, Kitula Yango alisema matarajio yao ni kwamba Swissport itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na weledi wa hali ya juu ili iweze kuendelea kuwahudumia kila wakati.
Amesema anatumaini kuwa kampuni hiyo itazingatia kila kilichokuwepo kwenye mkataba ikiwamo kutochelewesha ndege bila sababu ya msingi.
No comments:
Post a Comment