Adbox

Sunday, December 8, 2019

Marekani na Iran zabadilishana wafungwa

Iran imemuachilia mtafiti mmoja wa Marekani aliyeshtakiwa kwa upepelezi ili kubadilishana na mwanasayansi aliyepatikana na hatia ya ukiukaji wa vikwazo vya Marekani, pande zote mbili zimetangaza hapo jana.

Ubadilishanaji huo ulikuwa kwa malengo ya kidiplomasia yasio ya kawaida uliowezeshwa na Uswisi, huku Marekani ikiendeleza vikwazo vikali dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa Kinyuklia.

Raia huyo wa Marekani aliyezaliwa nchini China Xiyue Wang, mwanafunzi wa historia katika chuo kikuu cha Princeton alikamatwa mwaka 2016 na kuhukumiwa hadi miaka 10 gerezani kwa kosa la upepelezi.

Wang alikanusha madai yote,Wang aliachiliwa huru katika hatua ya ubadilishanaji wa wafungwa nchini Uswisi ili kuwezesha kuachiliwa kwa Massoud Soleimani, mwanasayansi wa Iran aliyekamatwa mwaka 2018 na kushtakiwa kwa kujaribu kuingizia kimagendo vifaa vya kimatibabu nchini Iran hivyo basi kukiuka vikwazo vya Marekani.

No comments:

Post a Comment

Adbox