Na Amiri kilagalila-Njombe
Wimbi kubwa la wasomi waliopo mitaani kwa kukosa ajira nchini limetajwa kusababishwa na vijana wengi kutozingatia kile wanachofundishwa vyuoni na badala yake kujikuta wakihitimu elimu ya juu pasina kujua nini watakwenda kufanya wawapo uraiani.
Katika mahafali ya 16 ya chuo cha ufundi cha manamba mpechi kilichopo mjini Njombe mhadhiri wa vyuo vikuu nchini kwa ngazi ya udaktari dokta Rechion Kimilike ambaye alikuwa mgeni wa heshima amesema kuwa vijana takribani milioni kumi kila mwaka wanaingia katika soko la ajira lakini waliowengi hawana stadi za maisha wala stadi za kazi jambo linalosababisha wengi wao kukata tamaa pale wanapokosa ajira.
“Vijana wa sasa hivi ni wanyonge hawajiamini katika maisha yao na kukosa kujiamini kunawasukuma kuingia kushiriki katika mambo machafu na mambo ya fujo,wengine wameingia katika hali hatari zaidi na mbaya zaidi wengine wanakuwa ni wahanga na kuwa zana za vurugu za kidini au fujo za kisiasa,hivyo vijana wetu wanapokosa ajira ni tishio la utulivu wa kisiasa”anasema Kimilike
Mkuu wa chuo hicho bwana Daniel Ole M'bezi anasema mbali na chuo hicho kukabiliwa na changamoto mbalimbali lakini kimefanikiwa kupata uwakala toka chuo cha usafirishaji taifa NIT kwa ajili ya kutoa mafunzo ya udereva ambao utamsaidia mwanachuo kupata ajira serikalini.
Joseph Lutumo,Charity Julius na Mary Makundi ni wahitimu wa elimu ya ufundi katika chuo hicho wanakiri kuwa ujuzi waliojifunza kwa kipindi chote utakwenda kuondoa kabisa changamoto ya kutegemea ajira serikalini kwani wanaweza kuitumia elimu hiyo kwa kubuni miradi mbalimbali.
Regina Lindi anawakilisha kundi la wazazi wa wanafunzi hao ambaye anasema hatarajii kuona vijana wao wanakwenda kujiingiza katika makundi yanayokinzana na tabia njema huku wakitaka gharama walizozitumia kuwasomesha zirejeshwe kwa kwenda kuchapa kazi kwa bidii.
Jumla ya wahitimu wanaopindukia 96 wa kozi mbalimbali wamefanikiwa kuhitimu masomo yao katika fani mbalimbali ikiwemo utalii katika chuo hicho.
Monday, November 11, 2019
Wasomi wanapokosa ajira husababisha tishio la kukosekana utulivu wa kisiasa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment