Adbox

Monday, November 11, 2019

Dkt Tulia Ackson ataka vijana kutumia mda wao vizuri na kuacha kuchati ovyo

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe,Tulia Ackson amewataka vijana kuacha kupoteza Muda Mwingi kutumia  kuchati kwenye Mitandao ya kijamii  na badala yake wanatakiwa kuitumia vyema kwa ajili ya kujiletea Maendeleo.

Mhe.Ackson ameyasema hayo  jijini Dodoma katika Kongamano la mdahalo wa Wanafunzi wa Vyuo vikuu ,mkoani hapa lijulikanalo kama

,IBUA lilioandaliwa na mfuko wa Kuendeleza Sekta za kifedha Tanzania, Financial Sector Deeping Trust (FSDT).

Mhe.Ackson amesema changamoto kubwa ambayo ipo kwa vijana wa sasa ni matumizi ya Mitandao vibaya badala ya kuitumia mitandao hiyo katika kuwaletea maendeleo.

“Sisi vijana unakuta anachati asubuhi mpaka jioni na hanufaiki na chochote ,siku hizi kumekuwa na Mchepuko tu wa kufungua magroup kwenye

 whasaap ili awe na yey admin,Vijana tumieni simu kama sehemu ya kufungua fursa na si kwa mawasiliano pekee”amesema Dkt Tulia.

Aidha Mhe.Ackson amesema vijana hawatakiwi kuwa watazamaji tu kwa mambo yanayoendelea bali wanatakiwa kuwa sehemu ya mambo hayo hususan ushiriki wa mambo mbalimbali ya maendeleo huku akiwataka kuwa na

malengo ya dhati pindi wanapoanzisha mradi na kusisitiza kuwa jambo la kwanza katika kufanikisha malengo ni kuwa na wazo na kufuatiwa na mtaji.

“Vijana kuwa hawana mitaji lakini kikubwa kinachohitajika ni wazo  na sio mtaji,unakopa kwa ajili ya nini"?amesema. Katika hatua nyingine Mhe. Ackson amewataka vijana kuacha kubishana na watu waliofanikiwa  na badala yake kuutumia muda wao vyema kuchapa kazi za kuwaletea Maendeleo.


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa Kuendeleza Sekta za kifedha Tanzania[FSDT]Sosthenes Kewe amesema lengo la Mdahalo huo ni kuwaanda vijana kuwa  viongozi wazuri katika taasisi za kifedha huku

akisema asilimia 86% ya Watanzania Wote wanaishi katika Maeneo yenye huduma za kifedha kila baada ya umbali wa kilometa 5.

Katika Mdahalo huo uliokwenda sambamba na Mada isemayo”Je,Taasisi Za

kifedha zina mchango gani katika kumwezesha msichana na Mvulana?Faustine Edward kutoka chuo cha St.John ameibuka kuwa Mshindi, Kongamano la Mdahalo wa vyuo vikuu mkoani Dodoma maarufu IBUKA limeenda

limekwenda na kaulimbiu isemayo ",Naweza,Nafanya,Nashinda".

No comments:

Post a Comment

Adbox