Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kutoa shilingi milioni 31 kwa shule ya Sekondari Misungwi ili kukamilisha ujenzi wa bweni linalojengwa na shule hiyo.
Waziri Ndalichako ametoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki alipofika shuleni hapo kukagua miundombinu ya shule hiyo ambapo Serikali imejenga madarasa mapya, maabara na Bweni yaliyowezesha wanafunzi kuongeza ari ya kusoma na kupelekea shule hiyo Kuongoza katika mtihani wa kidato cha sita Mkoani Mwanza na kuongeza idadi ya wanafunzi.
Ndalichako akiwa shuleni hapo amesema amefurahishwa kuona uongozi wa shule hiyo umekuwa ukitumia fedha vizuri na kuweka akiba kidogokidogo kwa miaka mitatu ambapo kupitia kupitia akiba hiyo wamepata fedha ambazo zimewawezesha kuanza ujenzi wa bweni jipya.
“Nimefurahishwa na mpango wa shule wa kuhifadhi fedha kidogo kidogo mpaka wamepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wa kike jitihada hizi ni lazima ziungwe mkono nami nikiwa waziri mwenye dhamana ya elimu natoa ahadi ya kuleta fedha za kumalizia huu ujenzi ” Alisema waziri Ndalichako.
Profesa Ndalichako amesema pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi pia atahakikisha samani za bweni hilo jipya zinanuliwa ili likamilike na kutumika kwa wakati.
Aidha, Waziri Ndalichako amewata wanafunzi katika shule hiyo kuzingatia masomo na kutojiingiza katika mambo ambayo yatawakatisha masomo na mwisho kutofikia ndoto zao.
Mkuu wa Shule ya sekondari Misungwi Mwanani Asembandwa amemshukuru Waziri wa Elimu kwa kutambua jitihada za shule za kuweka fedha kidogokidogo kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana
Monday, November 11, 2019
Serikali yaahidi kutoa Milioni 13 kukarabati shule hii
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment